SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA DAY 5

SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
IJUMAA, 9 JANUARI 2026
MOYO WA IBADA NA KUMTUMAINI MUNGU 🙏🔥

1️⃣ Omba Moyo wa Ibada na Shauku ya Kweli ya Kumwabudu Mungu
Omba Mungu akujalie moyo wa ibada ya kweli—kumwabudu katika roho na kweli katika mwaka huu wa 2026.
📖 Warumi 12:1; Yohana 4:23
Omba kinyume na roho ya ukawaida, mazoea, na ibada isiyo na uhai.
Ombea ibada zote za kanisa katika mwaka 2026 ziwe na upako, zijazwe uwepo wa Mungu, na ziletwe mabadiliko ya maisha.

2️⃣ Omba Moyo wa Kumtegemea Mungu kwa Moyo Wako Wote
Omba Mungu akupe imani ya kumtegemea Yeye pekee, kulingana na kaulimbiu ya DPC kwa mwaka 2026.
📖 Mithali 3:5; Yeremia 17:5–7; Zaburi 25:1–3

3️⃣ Omba Msaada na Uongozi wa Mungu Katika Maisha Yako Yote
Omba Mungu akupe msaada Wake wa kudumu na uongozi Wake katika kila eneo la maisha yako mwaka huu wa 2026.
📖 Mithali 3:6; Zaburi 121:1–2; Wakolosai 3:23–25

🙏 Tumtafute Bwana kwa mioyo ya unyenyekevu, tukimtumaini kikamilifu katika mwaka huu mpya.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top