SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA SIKU YA KUMI

SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
JUMATANO, 14 JANUARI 2026
MAHUSIANO, NDOA NA FAMILIA

1.⁠ ⁠Ombea Ndoa Zote za DPC
Mshukuru Mungu kwa ndoa zote zilizofungwa mwaka 2025.
Omba ndoa ziongozwe na upendo wa kweli. (1 Wakorintho 13:4–8)
Ombea uaminifu, furaha na amani katika ndoa; kataa mafarakano na magomvi.
Ombea ndoa ziwe ushuhuda na kielelezo bora kwa jamii na kuwavuta wengine kwa Kristo. (Mhubiri 4:9–12)
Omba Mungu awajalie mahitaji yote ya ndoa: watoto, uchumi na ustawi wa maisha.

2.⁠ ⁠Ombea Vijana Walioko Kwenye Mahusiano na Wanaotarajia Kuingia Kwenye Mahusiano
Omba vijana wawe na hofu ya Mungu na mioyo ya kumcha Bwana.
Omba Roho Mtakatifu awaongoze kuishi kwa hekima na kujiepusha na vishawishi vinavyobomoa familia.
(Zaburi 78:4–7; Zaburi 127:1; Tito 2:3–8)

3.⁠ ⁠Ombea Familia Yako
Ombea wazazi, ndugu na jamaa zako.
Ombea umoja na upendo katika familia; kataa mafarakano ya kindugu. (Zaburi 133)
Ombea tunda la Roho lionekane katika familia. (Wagalatia 5:22)
Omba ulinzi wa Mungu juu ya familia yako. (Zaburi 121:7–8)
Omba afya njema; simama kinyume na roho za magonjwa. (Kumbukumbu la Torati 7:15)

4.⁠ ⁠Ombea Mungu Apanue Mipaka ya Familia, Ndoa na Vijana
Omba baraka na ustawi wa jumla. (3 Yohana 1:2)
Omba Mungu apanue mipaka yako na ya familia yako. (1 Nyakati 4:10; Isaya 54:1–4)
Omba mkono wa Mungu ukuongoze na kukuinua katika kila eneo la maisha.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top