SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA DPC SIKU YA 11

SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA DPC – ALHAMIS 15 JANUARI 2026.
WATOTO, VIJANA, HUDUMA ZA SHULENI NA VYUONI

1.⁠ ⁠Ombea ulinzi wa kimwili, kiroho, na kiakili juu ya watoto na vijana.
•⁠ ⁠Kemea roho za uharibifu, tabia hatarishi zinazoathiri kizazi cha sasa. Ombea wazazi, walezi na kanisa watimize wajibu wao wa malezi ya watoto. Zaburi 121:7–8
•⁠ ⁠Ombea haki za Watoto na vijana katika mazingira wanayoishi na kusoma

2.⁠ ⁠Ombea vijana waliomaliza vyuo wapate fursa mbalimbali (Kazi/biashara) za kuendeleza Maisha yao.
•⁠ ⁠Waombee wapate mazingiza sahihi ya kutumia vipaji na elimu zao kwa ubunifu ili kujiendeleza kiuchumi iwe kazini au kujiajiri.
•⁠ ⁠Pinga roho ya kukata tamaa na msongo wa mawazo ndani yao. • Mithali 22:6 • Yeremia 29:11

3.⁠ ⁠Ombea uamsho wa kiroho miongoni mwa watoto na vijana.
•⁠ ⁠Ombea uamsho wa kiroho kwa wazazi na walezi ili washirikiane na kanisa, shule, vyuo, na jamii katika malezi ya watoto na vijana.
•⁠ ⁠Ombea program za Watoto na vijana na idara zikalete matokea chanya kwenye Maisha yao.
•⁠ ⁠Ombea Ubunifu katika kupanga program za Watoto na vijana

4.⁠ ⁠Ombea walimu na maslahi yao ya kiuchumi ili wafanya kazi kwa moyo wakiwalea na watoto na vijana huko mashuleni na vyuoni.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top