SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA SIKU YA 15

SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
JUMATATU, 19 JANUARI 2026

OMBI KUU: MAENDELEO YA WATU, KANISA NA PAG TANZANIA

1. Shukrani kwa Maendeleo

  • Mshukuru Mungu kwa maendeleo aliyokupa binafsi na kwa Kanisa katika mwaka 2025.
    Zaburi 126:3, Zaburi 103:1–5
  • Mshukuru Mungu kwa ajili ya Kanisa la DPC na umwamini kwa maendeleo makubwa zaidi katika mwaka 2026. Yeremia 29:11

2. Maombi kwa Uchumi na Kazi Zetu

  • Ombea uchumi wako; muombe Mungu abariki kazi za mikono yako na akufungulie milango ya fursa mbalimbali. Kumbukumbu la Torati 28:12, Wafilipi 1:6
  • Ombea eneo lako la kazi, biashara zako na miradi yako yote. Kumbukumbu la Torati 24:19–22
  • Simama kinyume na roho ya umaskini katika maisha yako. Mithali 10:22, , 1 Nyakati 4:10

3. Maombi kwa Maendeleo ya Kanisa la DPC

  • Ombea maendeleo ya DPC katika kila eneo.
  • Ombea miradi ya DPC, ikiwemo Multipurpose Building na eneo la Mkuranga kwa ajili ya miradi ya Shule na Chuo; muombe Mungu atupatie rasilimali za kutosha kuwezesha na kuendeleza miradi hii.
  • Ombea watu wa Mungu wawe na moyo wa kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu katika Kanisa la DPC. Zaburi 133; Waefeso 4:1–4
  • Simama kinyume na roho ya umaskini ndani ya Kanisa la DPC.

4. Maombi kwa PAG Tanzania

  • Ombea Halmashauri Kuu na Kamati Tendaji ya Taifa ya PAG Tanzania, ili Mungu awajalie umoja na hekima katika kufanya maamuzi ya busara kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa kwa utukufu wake. Yakobo 1:5
  • Ombea viongozi wote wa PAG Tanzania kuanzia ngazi ya kanisa la mahali hadi Taifa, Mungu awape umoja wa Roho na nia moja katika kutekeleza Mpango Mkakati. , Zaburi 133
  • Ombea maendeleo ya miradi mbalimbali ya PAG Tanzania, na mshukuru Mungu kwa neema ya kununua ekari 50 huko Itigi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Umisheni na Maendeleo ya Jamii.

5. Maombi kwa ajili ya maendeleo ya Mwili wa Kristo nchini Tanzania

  • Ombea Kanisa la Kristo nchini Tanzania likue, kwa umoja, ukomavu wa kiroho, na mabadiliko yatakayochochea ukuaji endelevu wa Kanisa.
    ·  Ombea hekima kwa taasisi zinayounganisha Kanisa kama CPCT, ili iwe ya kumtukuza Kristo, kuimarisha umoja wa Mwili wa Kristo, na kuchangia maendeleo ya Kanisa nchini Tanzania.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top