SIKU 21 ZA KUOMBANA KUFUNGA – JUMAMOSI 15, 2026
OMBI KUU: USHIRIKA WENZA NA USHIRIKIANO
1. Maombi binafsi
• Mshukuru Mungu ushirikiano mzuri ulionao na familia yako.
• Mshukuru Mungu kwa mahusiano mazuri na watu wengine katika maisha ya kila siku – waamini wenzako, wafanya kazi wenzako, majirani Mithali 27:17.
• Omba utulivu, umoja, mshikamano na upendo katika familia yako
Isaya 32:18; Wakolosai 3:15
2. Mshukuru Mungu kwa kukupa nafasi ya kuhudumia wengine.
• Mshukuru Mungu kwamba amekuwezesha kuwahudumia wengine kiroho, kimwili na kijamii Mathayo 5:9; 25:34 – 36
• Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kushiriki katika kazi ya Bwana kupitia kanisa la DPC Wafilipi 1:3 – 5
• Omba kwamba Mungu aendelee kukutumia kwa ajili ya utukufu wake Wafilipi 1:6
3. Mshukuru Mungu kwa ushirika wa DPC na makanisa mengine.
• Mshukuru Mungu kwa ushirikiano wa PAOC katika kuwezesha kazi ya Mungu Tanzania na Africa.
• Omba kwama kanisa la Tanzania ikiwemo PAGT litaendelea kukua kihuduma na kuyafikia mataifa mengine Mathayo 28:19 – 20
• Omba kwa ajili ya Mwanza Christian College kiweze kuandaa watumishi wengi wa injili Waefeso 4:11 – 13
4. Omba kwa ajili ya makanisa yote ambayo yamejitoa kuhubiri Injili ya Kristo.
• Ombea CPCT (Council of Pentecostal ChurchesT in anzania) waweze kutimiza kusudi la Mungu katika makanisa ya kipentecoste 1Kor 12:4 – 6
• Omba roho ya ushirikiano katika kupeleka injili kwa wale ambao hawajafikiwa Warumi 12:14 – 15
5. Ombea ibada za Jumapili – Omba uwepo wa Mungu na nguvu za Roho Mtakatifu.

