SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA SIKU YA 16

SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
JUMANNE, 20 JANUARI 2026

OMBI KUU: UAMSHO NA KANISA

1️⃣ Ombea uamsho kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Omba Roho Mtakatifu awashe moto wa uamsho ndani yako na ndani ya kanisa kwa ujumla. Omba toba ya kweli, utakatifu, bidii ya maombi, ujazo wa Roho Mtakatifu, miujiza, na kumtumikia Mungu kwa uaminifu.
📖 Habakuki 3:2; Matendo ya Mitume 3:19; 4:31; Warumi 12:11

2️⃣ Ombea Roho wa maombi na udhihirisho wa nguvu za Mungu.
Omba Mungu amimine Roho wa neema na maombi juu ya watu Wake, ili udhihirisho wa nguvu za Roho Mtakatifu uwe wa kweli. Kemea kila nguvu za giza na kila roho inayopinga kazi na udhihirisho wa nguvu za Mungu.
📖 2 Wakorintho 10:1–5; Waefeso 6:18; LukOmbea wachungaji, walimu, wainjilisti, waimbaji, na watumishi wote wa Mungu wajazwe ujasiri na hekima ya kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu kwa usahihi na ujasiri, wakimtumikia Mungu kwa moyo wote.
📖 Waefeso 4:11–13; Matendo ya Mitume 4:31; 2 Timotheo 2:15; Yeremia; Matendo ya Mitume 4:31; 2 Timotheo 2:15; Yeremia 1:7–8

4️⃣ Ombea uamsho wa wokovu.
Ombea uamsho wa wokovu kwa watu wanaotuzunguka, Tanzania, na ulimwengu mzima—watu waokoke, wabatizwe, na waingizwe katika familia ya watoto wa Mungu.
📖Mathayo 28:19–20, Matendo ya Mitume 2:47, 1 Timotheo 2:3–4

Siku21ZaMaombi #KufungaNaKuomba #Uamsho #DPC #RohoMtakatifu #KanisaHai #Maombi

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top