SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA SIKU YA 19

SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
IJUMAA 23JAN 2026

 Kuwa na Imani Imara Katika Bwana.

  1. Mwambie Mungu ASANTE; Zab 52; 9
    Mshukuru Mungu kwa wema wake katika maisha yako.
    Mshukuru Mungu kwa neema yake katika maombi haya tangu siku ya kwanza hadi leo
  2. Mwombe Mungu akusaidie kuwa IMARA katika Imani itakayokuwezesha kukabiliana na changamoto za Kifamilia, maisha , majaribu nk.
    Omba uendelee kumtegemea Mungu katika majira yote.
    1 Wakorintho 16:13,  Yakobo 1:6, Wafilipi 4:1,
  3. Mwombe Mungu akusaidie kuamini na kusimama katika ahadi zake hata kama huoni matokeo kwa wakati huo.
    Omba tunda la Roho Mtakatifu liwe dhahiri katika maisha yako.
    Omba Mungu akupe uelewa wa neno lake na usipeperushwe na Imani potofu.  2 Wakorintho 5:7, 2 Wathesalonike 3;3, Wagalatia 5;22, 1 Wafalme 18; 44
  4. Kemea roho ya hofu, mashaka na kutoamini katika maisha yako.
    Omba Mungu akusaidie uwe na imani iliyo sahihi katika neno lake.
    Mwombe Mungu akupe kushinda kila aina ya vikwazo vya kiimani.
    Ombea Mwili wa Kristo kusimama imara katika Bwana na katika uwezo wa Nguvu zake.
    Marko 9:23, Wagalatia 5:22-23, Yakobo 1;5-7, Efeso 6:10

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top