SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA SIKU YA 20

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA – DPC: Jumamosi 24/01/2026

Ombi kuu: SIFA NA SHUKURANI

  1. Omba mbele za Mungu sawasawa na sala Yesu aliyowafundisha wanafunzi wake – Mathayo 6:9-13
  • Shukuru na kuendelea kuomba baraka na kibali cha Mungu maishani mwako, familia yako, na kanisa lako/DPC – Mithali 10:22

………………………………………………………………………………………………………………………………

2. Shukurani za binafsi – Zaburi 118:1

  • Mshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea 2025; na yale yote atakayokufanyia 2026
  • Mshukuru Mungu kwa zawadi ya wokovu na uhai
  • Mshukuru Mungu kwa kushiriki maombi ya siku 21
  • Mshukuru Mungu kwa mafanikio yote anayokupa – afya, kazi, elimu, uchumi, familia, huduma – Zaburi 111:1-2

3. Shukurani za kihuduma – Wakolosai 4:2 – 6

  • Mshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea 2025; na yale yote atakayokufanyia 2026
  • Mshukuru Mungu kwa zawadi ya wokovu na uhai
  • Mshukuru Mungu kwa kushiriki maombi ya siku 21
  • Mshukuru Mungu kwa mafanikio yote anayokupa – afya, kazi, elimu, uchumi, familia, huduma – Zaburi 111:1-2

4. Shukurani za kihuduma – Wakolosai 4:2 – 6

  1. Mshukuru Mungu kwa ajili ya Kanisa la DPC / PAGT. Omba kanisa liendelee kuitangaza injili ya Kristo 2026 / siku zote
  2. Mshukuru Mungu kwa ajili ya washirika na viongozi wote, na kuwatakia baraka za Mungu katika utumishi wao kwa Mungu
  3. Shukuru na kuomba neema ya Mungu juu ya DPC, na ufanisi katika mipango ya 2026 – Zaburi 136:1-4, Mithali 3:6

5. Mushukuru Mungu na uombe aendelea kuachilia uwepo wake katika ibaada zetu kila tunapokutana – Kutoka 33:12-15

  • Ombea ibaada zetu zote za Jumapili hii – kumbuka tutakuwa na ibaada ya kusifu na kuabudu ya kwanza 2026.

6. Sifu na kushukuru Mungu kwamba amesikia na kujibu maombi yetu yote tangu tulipoanza hadi leo – Mathayo 7:7-11

  • Mpe Mungu sifa na shukurani kutoka moyoni kwa kadri Roho Mtakatifu anavyokujalia – Zaburi 138:1-3
  • Tumshukuru Mungu kwa nyimbo za sifa na shukurani huku tukimtolea Mungu sadaka.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top