๐ย MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA NUSU MWAKA
Jumatatu, 13 Julai 2026
Tunakukaribisha kuanza wiki hii ya kufunga na kuomba kwa kumtafuta Mungu kwa moyo wote. Tuungane katika maombi tukimshukuru Mungu kwa uaminifu wake na kumkabidhi nusu ya pili ya mwaka 2026 mikononi mwake.
๐๏ธ 1. Maombi ya Shukrani
๐ Zaburi 103:1โ5; 1 Wathesalonike 5:16โ18
- Mshukuru Mungu kwa kutuvusha salama nusu ya kwanza ya mwaka 2026.
- Mshukuru kwa maisha yako, familia yako, kazi yako, na baraka zake nyingi.
- Mshukuru kwa ajili ya Kanisa lake.
- Mshukuru kwa ajili ya Taifa la Tanzania na ulimwengu mzima.
๐ 2. Mkabidhi Mungu Nusu ya Pili ya Mwaka 2026
๐ Mithali 3:5โ6; Zaburi 37:5; Isaya 43:18โ19
- Mwombe Mungu akuongoze, akufungulie milango mipya, na akatimize makusudi yake katika maisha yako.
๐ 3. Ombea Mahitaji ya Wiki Hii
๐ Wafilipi 4:6โ7; Yeremia 33:3
- Wasilisha mbele za Mungu mahitaji yako binafsi, ya familia, Kanisa, na Taifa, ukiamini kuwa Yeye husikia na kujibu maombi.
“Mkabilieni Mungu kwa imani, kwa maana Yeye ni mwaminifu na anaweza kufanya mambo mapya.”
#MidYearPrayerAndFasting #MaombiYaKufunga #DPCKinondoni #PrayWithoutCeasing #TrustTheLord #DarEsSalaamPentecostalChurch #Tanzania

