MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA KATIKATI YA MWAKA 2026 – UAMSHO

🔥 MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA KATIKATI YA MWAKA 2026

SIKU YA 2 | Jumanne, 14 Julai 2026

OMBI KUU: UAMSHO 🔥

“Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie?” — Zaburi 85:6

Leo tumwombe Mungu alete uamsho wa kweli ndani ya maisha yetu, familia zetu, na Kanisa Lake.

🙏 Ombea Uamsho Ndani Yako na Ndani ya Kanisa
• Uishi maisha ya utakatifu na kumcha Mungu (Matendo 10:1–2).
• Uwe mtu wa maombi na ujitoe kikamilifu kwa Mungu na kazi Yake.
• Umzalie Kristo matunda na ushiriki katika kulijenga Kanisa Lake (Matendo 9:31).
• Uamsho wa kweli ulete ukuaji wa kiroho, umoja, na kuimarisha Kanisa la Kristo.

🙏 Ombea Uamsho wa Karama na Vipawa
• Mungu achochee na kuhuisha karama zilizo ndani yako (2 Timotheo 1:6–7).
• Akupe ujasiri mpya wa kumtumikia kwa uaminifu (Matendo 3:6).
• Aachilie roho ya maombi ndani yako na ndani ya Kanisa (Matendo 12:5).
• Aondoe kila uovu na kila kizuizi kinachopinga kazi Yake (Matendo 13:6–12).

🙏 Ombea DPC
• Ombea moto mpya wa uamsho ushuke juu ya Dar es Salaam Pentecostal Church (DPC), viongozi wake, watumishi, idara zote, vikundi vyote vya huduma, na washirika wote.
• Mungu aliwezeshe Kanisa kutimiza kusudi Lake kwa nguvu za Roho Mtakatifu, umoja, na upendo.

“Ee Bwana, tuhuishe tena, ili jina Lako litukuzwe kupitia Kanisa Lako.” 🔥🙌

#MaombiYaKufungaNaKuomba2026 #SikuYa2 #Uamsho #TuhuisheTena #OmbaBilaKukoma #RohoMtakatifu #KanisaLaKristo #MotoWaUamsho #DPCKinondoni #DarEsSalaamPentecostalChurch #MwaminiAnayeomba #MtumainiBwana

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Discussion

  1. Micchael Paul

    Ubarikiwe sana.

Back to top

Share with