π MAOMBI YA KATIKATI YA MWAKA DPC
JUMATANO, 15 JULAI 2026
π¨βπ©βπ§βπ¦ KUOMBEA FAMILIA
“Bwana ndiye anapoijenga nyumba, wajengao wafanya kazi bure.” β Zaburi 127:1
I. MSHUKURU MUNGU KWA ZAWADI YA FAMILIA
π Zaburi 127:1β5
β
Mshukuru Mungu kwa zawadi ya familia na kwa kutufikisha hapa salama.
β
Mshukuru kwa ulinzi wake juu ya ndoa, watoto na wazazi wetu.
β
Mshukuru kwa rehema zake na uaminifu wake katika maisha ya familia zetu.
II. TUOMBE MUNGU ASHUGHULIKIE CHANZO CHA MATATIZO YA FAMILIA
π Mwanzo 37:3β4
π Omba Mungu aondoe kila mzizi wa upendeleo, wivu na chuki ndani ya familia zetu.
π Omba arejeshe upendo, mawasiliano mazuri na msamaha katika nyumba zetu.
π Omba atufanye kuwa watu wa upatanisho na amani kama Yusufu.
III. TUOMBE MUNGU ALINDE FAMILIA ZETU NA KUTIMIZA KUSUDI LAKE
π Zaburi 128:1β4; Mwanzo 50:20
π‘οΈ Omba Mungu alinde familia zetu na watoto wetu dhidi ya kila mpango wa adui.
π‘οΈ Omba atimize kusudi lake katika maisha ya kila mwanafamilia.
π‘οΈ Omba hofu ya Mungu itawale katika nyumba zetu.
IV. TUOMBE MUNGU ABARIKI NDOA, WATOTO NA UCHUMI WA FAMILIA
π Warumi 12:2
π Omba Mungu alinde na kuimarisha ndoa, awaongoze wanaotamani kuingia katika ndoa na kuwajalia wenzi wanaomcha Mungu.
πΆ Omba awakumbuke wanandoa wanaotamani kupata watoto, awalinde watoto wetu na wawakuzie katika hofu yake. (Zaburi 127:3β5)
πΌ Omba Mungu afungue milango ya uchumi, abariki kazi za mikono yetu na atupe hekima ya kusimamia alichotukabidhi. (Kumbukumbu la Torati 8:18)
Karibu tuungane katika maombi ya pamoja tukiiweka familia mbele za Mungu. Mungu anaweza kuleta uponyaji, upendo, umoja na baraka mpya katika kila nyumba.
#MaombiYaKatikatiYaMwaka#KuombeaFamilia#DPCKinondoni#DarEsSalaamPentecostalChurch#PrayerAndFasting#FamilyPrayer#Ndoa#Watoto#Familia#TrustTheLord#2026
MAOMBI YA KATIKATI YA MWAKA DPCJUMATANO, 15 JULAI 2026 – KUOMBEA FAMILIA

