MTAZAME YESU

UJUMBE: MTAZAME YESU
KITABU: HESABU 21:4-9
4 Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia.
5 Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.
6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.
7 Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
8 Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

HUKUMU KWA WANA WA ISRAEL (Mstari 6)

MUNGU ALITOA SULUHISHO

MTAZAME YESU

  1. AMINI NA WEKA TUMAINI LAKO KWA MUNGU
    YOHANA 3:14-17 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
    16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
    17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI

    WAEBRANIA 12:1-2 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
  2. AMINI NENO LA MSALABA
    1 WAKORINTHO 1:18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
    19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. 20 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22 Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; 23 bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi;
    24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. 25 Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu. UJUMBE WA MSALABA NI UPI?
    1 WAKORINTO 1:18

UJUMBE WA MSALABA
WAGALATIA 3:14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

2 WAKORINTHO 5:21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.

WAKOLOSAI 3:2-3
2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.
3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

MATENDO 17:28
28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

AMINI NA WEKA TUMAINI LAKO KWA YESU

  • YESU NI MWANZILISHI NA MWENYE KUTIMIZA IMANI YETU
  • YESU NI ALPHA NA OMEGA (MWANZO NA MWISHO)
  • YESU NI MCHUNGAJI MKUU NA MWEMA
  • YESU NI UFUFUO NA UZIMA
  • YESU NI MKATE WA UZIMA
  • YESU NI KUHANI MKUU
  • YESU NI MFALME WA WAFALME NA MUNGU MWENYE NGUVU
  • YESU NI EMMANUEL, MUNGU PAMOJA NASI
  • YESU NI MWOKOZI WETU NA MKOMBOZI WETU
  • KRISTO NI YOTE KATIKA YOTE
  • JINA LA YESU LAPITA MAJINA YOTE. NDANI YA JINA LAKE TUNA MAMLAKA NA NGUVU
  • YESU KRISTO NI NGUVU YA MUNGU NA HEKIMA. MWANGALIE YEYE, WEKA TUMAINI LAKO NDANI YAKE
×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top