MTUMAINI BWANA KWA MOYO WAKO WOTE

  1. Jifunze na utii neno la MUNGU
    Mithali 3:1-10

    1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.
    2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
    3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
    4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
    5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
    6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
    7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu.
    8 Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.
    9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
    10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

Yoshua 1:7-8
7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Yohana 14:23-24
23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

2. Rehema na kweli zisifarakane nawe
Wagalatia 5:22-23
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

3. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote.
Mithali 3:5-8 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.

4. Mtokee Bwana kwa moyo wa kupenda
2 Wakorinto 9:6-7 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top