USAJILI PROGRAM MAALUM YA SIKU YA FAMILIA 14 OKT 2026
WIKI YA FAMILIA YA DPC 2026: Huduma ya Wanandoa inayo furaha kutangaza kuwa Wiki ya Familia ya mwaka 2026 itafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 18 Oktoba 2026. Kauli mbiu – “Kutembea Pamoja na Mungu”: Kujenga Familia za Haki — Mika 6:8.
Wiki ya Familia ya mwaka huu italenga kuwakutanisha familia pamoja katika ibada, ushirika, mafundisho, na shughuli zenye maana zinazowahamasisha familia kumfuata Mungu, kujenga nyumba imara, zenye haki na zinazomweka Mungu kuwa msingi wa maisha ya familia. Ratiba ya wiki ni kama ifuatavyo:
- Jumanne, tarehe 13 Oktoba 2026 – Kutembea na Mungu kama familia, saa 11:30 jioni hadi saa 1:30 jioni.
- Jumatano, tarehe 14 Okt 2026 – Programu maalum ya Siku ya Familia.
- Alhamisi tarehe 15 Oktoba 2026 – Kulea watoto wanaojua njia za Mungu, saa 11:30 jioni hadi saa 1:30 jioni.
- Ijumaa, tarehe 16 Oktoba 2026 Maombi ya Pamoja, saa 11:30 jioni hadi saa 1:00 jioni.
- Jumapili, tarehe 18 Oktoba 2026 – Ibada za Jumapili
PROGRAMU MAALUM YA FAMILIA — Jumatano, tarehe 14 Oktoba, 2026
Programu maalum ya Siku ya Familia siku ya Jumatano, itafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Tutakuwa na wazungumzaji maalum watakaoshirikisha mafundisho na uzoefu wa vitendo kuhusu mada zifuatazo:
- Familia na Uponyaji wa Majeraha ya Kisaikolojia (Trauma)
- Fedha na Familia
- Familia na Teknolojia
Mchango wa chakula kwa ajili ya Siku ya hii maalum ya Familia ni TZS 6,500 kwa mshiriki mmoja. Michango itumwe kwa: Stephano Mwalukasa kupitia simu namba 0787 137 933.
Ili kuwa na maandalizi na mipango mizuri, washiriki wote na familia wanahimizwa kujiandikisha na kutoa michango yao mapema. Usajili na malipo vinaweza kufanyika kwa kuwasiliana na Stephano Mwalukasa kupitia 0787 137 933, au mara baada ya ibada.
Tunatazamia kusherehekea Wiki ya Familia 2026 pamoja!






