KUSUDI LA WOKOVU KWA MWAMINI

✨ KUSUDI LA WOKOVU KWA MWAMINI βœ¨πŸ“– 2 Wakorintho 5:14–21

Je, umewahi kujiuliza, Mungu alikuokoa kwa kusudi gani?
Wokovu si kwa ajili ya kusamehewa dhambi pekee au kujiandaa kwenda mbinguni. Mungu ametuokoa ili maisha yetu yawe ushuhuda wa neema yake na kutimiza kusudi lake hapa duniani.

1πŸ”Ή Mungu alituokoa ili ATUBADILISHE.
πŸ“– 2 Wakorintho 5:14–17; Yohana 3:3–7; Ezekieli 36:26–27; Matendo 9:1–22
Tunapompokea Kristo tunakuwa viumbe vipya. Maisha yetu hubadilishwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

2πŸ”Ή Mungu alituokoa ili ATUPATANISHE NAYE.
πŸ“– 2 Wakorintho 5:18–19; Isaya 59:1–2; Warumi 5:8; Luka 19:1–10

Kupitia Yesu Kristo, uhusiano uliovunjika kati ya mwanadamu na Mungu unarejeshwa.

3πŸ”Ή Mungu alituokoa ili TUMWAKILISHE DUNIANI.
πŸ“– 2 Wakorintho 5:20–21; Mathayo 5:16; Mathayo 28:18–20; Matendo 1:8

Sisi ni mabalozi wa Kristo, tukiitwa kuangaza nuru yake na kuwafikia wengine kwa Injili.

πŸ™ Hitimisho
Mungu hakukuokoa bila kusudi. Alikuokoa ili ubadilishwe, upatanishwe naye, na uishi maisha yanayomtukuza.

➑️ Kama bado hujampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, leo ni siku ya wokovu.

➑️ Kama umeokoka lakini umetembea mbali na kusudi la Mungu, leo mrejee Bwana kwa moyo wote. Yeye ni mwaminifu, mwenye rehema, na yuko tayari kukupokea tena.
Bwana atusaidie kuishi kusudi ambalo alituokoa kwa ajili yake. πŸ™

#DPC#DarEsSalaamPentecostalChurch#NenoLaMungu#Wokovu#YesuKristo#Imani#KusudiLaMungu#BaloziWaKristo#NeemaYaMungu#Uinjilisti

×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top

Share with