MTUMAINI BWANA KWA AJILI YA UKOMAVU WA KIROHO
MITHALI 3:5-6 MATENDO 2:42-47
Kumtumaini Mungu ni ile hali ya kumtegemea, kumtarajia, kumngojea, kumkiri, na kujiaminisha katika Yeye.
KUMTUMIKIA MUNGU ni kuwa na hakika katika Mungu – yaani:
- SIFA ZAKE: – Mwenye nguvu zote, Mwenye kujua yote, na Mwenye uwezo wa kuwa mahali popote – DANIEL 4:35
- AHADI ZAKE – zote ni Ndio na Amina – 2 WAKORINTHO 1:20
- MAWAZO & NJIA ZAKE – mawazo yake na njia zake sio mawazo yetu wala njia zetu – ISAYA 55:8-9
UKOMAVU WA KIROHO unatusogeza karibu na Mungu na ni kitu endelevu katika maisha ya ukiristo – WAFILIPI 3:12-14
UKOMAVU WA KIROHO wa Mkiristo unadhibitishwa kupitia maisha yake ya kila siku na hasa katika maeneo ya Kujifunza Neno la Mungu, Maisha ya Maombi, Ushiriki katika Vikundi vidogo, Utumishi wake kwa Mungu, na Uwakili mwema. – MATENDO 2:42- 47
- Tutazame kwa Pamoja eneo la MAOMBI KAMA KICHOCHEO MUHIMU CHA UKOMAVU WA KIROHO (somo la leo).
×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video







