IJUMAA 10 JAN 2025 KUYAJUA NA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU |
1.Omba Mungu kwamba mapenzi kamilifu ya Mungu kwa kanisa la DPC yafunuliwe na yatendeke kama shauri la Mbingu lilivyo. Waefeso 1:11, 5:15-17, Warumi 12:2. 2.Mwombe Mungu aongoze na kusimamia mchakato wako wa ukuaji, ili ukue na kuwa mkomavu kiasi cha kuweza kuyafanya mapenzi yake hata kama yatakugharimu kupoteza vitu fulani kama ilivyokuwa kwa watumishi wake wa zamani kama vile Ibrahimu, Yusufu, Danieli na wengine wengi . Wagalatia 1:4, Mwanzo 12:1,4, 39:9, Danieli 1:8, Mathayo 16:24-25. 3.Omba Mungu akupe uwezo wa kiroho wa kupambanua fursa zinazotoka kwake na zile zinazokuja kama mtego wa kukuondoa katika mpango wa Mungu. 1 Yohana 4:1-2, Yoshua 9:1-6,14, Mwanzo 18:1-5. 4.Ombea viongozi wa kanisa la PAG Tanzania katika ngazi zote kuyajua na kuyatenda mapenzi ya Mungu katika huduma zao.Wakolosai 1:9-10, Yeremia 23:21-22, Waefeso 4:11-14, Warumi 10:2. |