SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA 21 JANUARI 2025 – MAOMBI KWA KANISA LA KRISTO TANZANIA NA DUNIANI KOTE.

1. Ombea kanisa (mwili wa Kristo) la Tanzania ili kuhubiri  Injili sahihi ya wokovu na kusimama mahali palipobomoka  kama sauti ya kitume na kinabii likitimiza wajibu wake kama nuru na chumvi ya ulimwengu.  Isaya 58:12,Matendo 1:8 ,Isaya 6:1-8 , Yohana 20:21 , Isaya 52:7 

2. Ombea jumuia zote za makanisa hapa Tanzania: Tanzania Episcopal Council (TEC), Christian Council of Tanzania (CCT), Council of Pentecostal Churches in Tanzania (CPCT), Seventh Day Adventist (SDA) ziendelee kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa katiba zao kiufanisi zaidi. 

3. Ombea watakatifu wote duniani, hasa wale wanaopitia katika mateso kwa ajili ya imani yao, Mungu azidi kuwapa ujasiri, kuwaimarisha na kuwatumia kama chumvi na nuru ya ulimwengu 

– Ombea kazi ya umisheni duniani kote

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top