✨ SIKU 21 ZA MAOMBI NA KUFUNGA – DPC ✨Jumatatu, 5 Januari 2026. Maelekezo ya Maombi (Siku ya 1):
1️⃣ Omba toba na rehema mbele za Mungu kwa ajili yako, familia yako, ukoo wako, kanisa lako, na nchi yako, ili Mungu aendelee kuturehemu. 📖 1 Yohana 1:8–10; Zaburi 51:1–10
2️⃣ Jinyenyekeshe na kujidhabihisha mbele za Mungu, ili akupe neema ya kuomba sawasawa na mapenzi yake.
📖 1 Petro 5:5–7
3️⃣ Omba kinyume na vikwazo vyote vya shetani vinavyoweza kukuzuia au kukufanya usishiriki katika siku hizi 21 za maombi. 📖 Yakobo 4:7–10
4️⃣ Omba kwa unyenyekevu Mungu asikie na kujibu maombi yako yote.
📖 2 Nyakati 7:14; Ezra 8:21–23
SIKU 21 ZA MAOMBI NA KUFUNGA – DPC

