🙏 SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
JUMANNE | 6 JANUARI, 2026
🕊 SHUKRANI NA MAOMBI BINAFSI
1️⃣ Maombi ya Shukrani
• Mshukuru Mungu kwa kukuvusha salama mwaka 2025 na kukuingiza 2026
📖 Zaburi 103:1–14
• Mshukuru Mungu kwa jinsi alivyokuwezesha kutimiza malengo yako na kwa kila baraka ya rohoni na ya mwilini kwako na familia yako
📖 Yakobo 1:17 | Zaburi 126:3
• Mshukuru Mungu kwa neema na rehema zake juu yako na juu ya taifa la Tanzania
📖 Maombolezo 3:22–23 | Waefeso 3:20
2️⃣ Maombi Binafsi
• Ombea mipango yako binafsi na ya familia kwa mwaka 2026
📖 Wafilipi 4:19 | Yeremia 30:17
🙏 Tunapomshukuru Mungu, tunafungua mlango wa baraka mpya.







