SIKU 21 ZA MAOMBI NA KUFUNGA IJUMAA 16 JANUARI 2026.
๐ MAOMBI KWA AJILI YA JAMII YETU ๐
Leo tunasimama kidete kuwaombea wale walio karibu nasi na wenye uhitaji maalum. Ungana nasi katika mambo haya manne:
1๏ธโฃ Wenye Uhitaji Maalum: Tuwaombee Wazee, Wajane, Yatima, na Walemavu. Mungu akutane na mahitaji yao ya kila siku. ๐ Zab 145:14-16, Eze 22:30, Mit 31:20
2๏ธโฃ Kanisa Kuhudumia Jamii: Tuombe Mwili wa Kristo upate neema ya kuwagusa wahitaji kwa utukufu wa Mungu. ๐ Kum 15:11, Mit 14:31
3๏ธโฃ Mungu Akutumie Wewe: Omba Mungu akufanye kuwa chombo cha baraka kwa jamii inayokuzunguka. Usipite pembeni, kuwa jibu la maombi yao. ๐ Mit 22:2, 21:13
4๏ธโฃ Shukrani kwa Wanaojitoa: Tunawashukuru na kuwaombea watu wote na vikundi vinavyojitoa kuhudumia jamii kwa hali na mali. ๐ Yakobo 1:27, Mdo 20:35

