SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
JUMATANO, 21 JANUARI 2026
OMBI KUU: TANZANIA NA MATAIFA MENGINE 🇹🇿🌍
1️⃣ Shukrani kwa baraka za Tanzania. 📖 Zaburi 104:14–15; Yeremia 5:24
• Mshukuru Mungu kwa nchi nzuri yenye rasilimali nyingi.
• Mshukuru Mungu kwa amani na uhuru wa kuabudu tulio nao Tanzania.
2️⃣ Omba umoja, upendo, amani na haki vitawale. 📖 Mika 6:8; Zaburi 133:1–3
• Omba kinyume na roho ya migawanyiko katika taifa letu.
• Omba tofauti za kisiasa na imani za kidini zisitugawanye kama Watanzania.
• Omba roho ya upendo kwa Watanzania na wageni wote wanaoishi nchini.
3️⃣ Ombea viongozi wa nchi kuongoza kwa hekima na uadilifu.📖 1 Timotheo 2:1–4; Danieli 9:3–5
• Ombea viongozi wa serikali na vyama vya siasa: Rais, Bunge, Baraza la Mawaziri, Mahakama, Wakuu wa Mikoa.
• Ombea viongozi wa kidini wawe chachu ya upendo na umoja.
• Omba hofu ya Mungu kwa viongozi wetu.
4️⃣ Omba amani kwa Afrika na mataifa mengine.📖 Nehemia 1:4–5; Mithali 6:16–17
• Ombea amani na utulivu Uganda baada ya uchaguzi.
• Ombea mataifa yanayopitia vita: Congo, Sudan, Israel & Palestina, Urusi & Ukraine, n.k.
• Kemea roho ya vita na umwagaji wa damu.







