SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA SIKU YA 18

SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
ALHAMISI, 22 JANUARI 2026
🎯 OMBI KUU: MAHITAJI BINAFSI

1️⃣ Kumjua na Kumpenda Mungu
•⁠ ⁠Omba neema ya kumjua Mungu binafsi na kumpenda kwa moyo wako wote (Mathayo 22:37).
•⁠ ⁠Omba Mungu akusaidie kumtumikia kwa moyo mpya, kwa uaminifu na bidii katika maisha yako ya kila siku. (Warumi 12:11).
•⁠ ⁠Ombea kazi zako, huduma, na majukumu ya kila siku uyatimize kwa ubora na kwa nguvu za Roho Mtakatifu. (Wakolosai 3:23).

2️⃣ Maombi kwa Ajili ya Familia Zetu
•⁠ ⁠Omba kwa ajili ya wazazi, watoto, wenzi wa ndoa, na wakwe. (Yoshua 24:15).
•⁠ ⁠Omba Mungu abariki familia yako katika kila eneo—kiroho, kimwili, kijamii, na kiuchumi. (Zaburi 128:1–4).
•⁠ ⁠Omba upendo wa kweli, amani, na umoja katika familia zako. (Wakolosai 3:14–15).

3️⃣ Kuomba Kinyume na Nguvu za Giza
•⁠ ⁠Omba kinyume na nguvu zote za giza na mipango yote ya Ibilisi dhidi ya maisha yako. (Luka 10:19).
•⁠ ⁠Kataa hofu, uvivu, kukata tamaa, na kila kitu kinachoweza kuzuia mafanikio yako mwaka 2026. (2 Timotheo 1:7).
•⁠ ⁠Omba ulinzi wa Mungu juu ya mipango yako, kazi zako, masomo, na huduma yako. (Isaya 54:17).

4️⃣ Ulinzi, Afya, na Nguvu kwa Mwaka 2026
•⁠ ⁠Omba ulinzi wa Mungu katika mwaka mzima wa 2026. (Zaburi 91:10–12).
•⁠ ⁠Kemea ajali, magonjwa, udhaifu, na hatari zote kwa jina la Yesu.
•⁠ ⁠Omba afya njema, nguvu, imani, na ujasiri kila siku. (Isaya 40:31).
•⁠ ⁠Omba kwa imani, ukimwamini Mungu akupe uwezo wa kufanya yote katika Kristo anayekupa nguvu. (Wafilipi 4:13).

🙏 Tuombe pamoja, tukimwamini Mungu kwa ushindi kamili katika maisha yetu binafsi mwaka 2026.

Siku21ZaKuombaNaKufunga #DPC #MahitajiBinafsi #PrayerAndFasting #2026KwaYesu

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top