SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA – DPC: Jumamosi 24/01/2026
Ombi kuu: SIFA NA SHUKURANI
- Omba mbele za Mungu sawasawa na sala Yesu aliyowafundisha wanafunzi wake – Mathayo 6:9-13
- Shukuru na kuendelea kuomba baraka na kibali cha Mungu maishani mwako, familia yako, na kanisa lako/DPC – Mithali 10:22
………………………………………………………………………………………………………………………………
2. Shukurani za binafsi – Zaburi 118:1
- Mshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea 2025; na yale yote atakayokufanyia 2026
- Mshukuru Mungu kwa zawadi ya wokovu na uhai
- Mshukuru Mungu kwa kushiriki maombi ya siku 21
- Mshukuru Mungu kwa mafanikio yote anayokupa – afya, kazi, elimu, uchumi, familia, huduma – Zaburi 111:1-2
3. Shukurani za kihuduma – Wakolosai 4:2 – 6
- Mshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea 2025; na yale yote atakayokufanyia 2026
- Mshukuru Mungu kwa zawadi ya wokovu na uhai
- Mshukuru Mungu kwa kushiriki maombi ya siku 21
- Mshukuru Mungu kwa mafanikio yote anayokupa – afya, kazi, elimu, uchumi, familia, huduma – Zaburi 111:1-2
4. Shukurani za kihuduma – Wakolosai 4:2 – 6
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya Kanisa la DPC / PAGT. Omba kanisa liendelee kuitangaza injili ya Kristo 2026 / siku zote
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya washirika na viongozi wote, na kuwatakia baraka za Mungu katika utumishi wao kwa Mungu
- Shukuru na kuomba neema ya Mungu juu ya DPC, na ufanisi katika mipango ya 2026 – Zaburi 136:1-4, Mithali 3:6
5. Mushukuru Mungu na uombe aendelea kuachilia uwepo wake katika ibaada zetu kila tunapokutana – Kutoka 33:12-15
- Ombea ibaada zetu zote za Jumapili hii – kumbuka tutakuwa na ibaada ya kusifu na kuabudu ya kwanza 2026.
6. Sifu na kushukuru Mungu kwamba amesikia na kujibu maombi yetu yote tangu tulipoanza hadi leo – Mathayo 7:7-11
- Mpe Mungu sifa na shukurani kutoka moyoni kwa kadri Roho Mtakatifu anavyokujalia – Zaburi 138:1-3
- Tumshukuru Mungu kwa nyimbo za sifa na shukurani huku tukimtolea Mungu sadaka.

