MAMBO YA KUOMBEA JUMAMOSI: 16 JANUARI 2021

WIKI MBILI ZA KUFUNGA NA KUOMBA: DPC
11-23 Januari 2021

MAMBO YA KUOMBEA: JUMAMOSI 16/1/2021

  1. Omba Roho Mtakatifu ambaye ndiye msaidizi wetu akupake mafuta na akujaze nguvu zake na akusaidie kutimiza kusudi la Mungu. Yohana 14: 16,26, Matendo 1: 8, Zekaria 4: 6-7

• Omba kwamba mito ya maji ya uzima itatiririka kutoka ndani yako.
Yohana 7:37-38,

•Omba kwamba uzae tunda la Roho. Wagalatia 5: 22-23

•Omba kwamba Roho Mtakatifu akupake mafuta na kukupa nguvu ya kufanya mambo zaidi ya uwezo wa kibinadamu.
Isaya 11:2, Matendo 2:17-18

  1. Ombea DPC kuwe na udhihirisho wa nguvu za Mungu katika huduma zote za kanisa.
    Omba udhihirisho wa uwepo wa Mungu katika huduma na vipindi vyote tunapokusanyika. Omba kwamba kila muumini akutane na nguvu ya Roho Mtakatifu inayobadilisha. Matendo 4:31,
    1 Wakorintho 12: 8-1.
  2. Ombea uamsho katika mwili wa Kristo. Omba urejesho wa nguvu za Mungu katika kanisa
    1 Wakorintho 2: 4-5; 4:20, Waefeso 1: 15-20.
    Tangaza kwamba Yesu analijenga kanisa lake na malango ya kuzimu hayatalishinda. Mathew 16: 18
  3. Mshukuru Mungu kwa upako wa Roho Mtakatifu katika maisha yako. Mshukuru Mungu kwa sababu utazaa matunda katika kile unachofanya kwa sababu umewezeshwa na ufahamu na hekima itokayo juu. Isaya 61: 1-2

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top