MSHUKURUNI BWANA KWA KUWA NI MWEMA

MSHUKURUNI BWANA
KWA KUWA NI MWEMA

KITABU
ZABURI 118:1-24

Daudi anazigawanya sababu
za kumshukuru Mungu katika makundi mawili

I. Kwakuwa Bwana ni mwema

II. Kwa maana Fadhili za Bwana ni za milele

Zaburi 118:2 ñ 4

Israeli
Malango ya Haruni/makuhani

Wamchao Bwana wote
2 ìIsrael na aseme sasa
Fadhili zake ni za mileleî

3 ìmalango ya Haruni na waseme sasa
Fadhili zake ni za milele.î

4 ìWamchao Bwana na waseme sasa
Fadhili zake ni za mileleÖ.î

  1. Huyashibisha matakwa ya moyo wako
  2. Bwana hujibu maombi yako

3.Bwana ni mlinzi wako

  1. Bwna ni msaidizi wako Zaburi. 118:Nyuki hufa baada ya kumgíata mtu:

Lesson: ìNao watapigana naw; lakini hawatakushindaî maana Bwana yuko Pamoja nawe kushindana na wanaoshindana nawewe (Jer. 1:19)

Hitimisho
i. Mshukuru Mungu
kwa kukupatia ushundi

II. Kiri kwa ushindi ambao
Bwana anakwenda kukupatia.

Zaburi 118:1 ñ 24
1 Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2 Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

3 Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

4 Wamchao Bwana na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

5 Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.

6 Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

7 Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.

8 Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.

9 Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.

10 Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

11 Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

12 Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia.

14 Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.

15 Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.

16 Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.

17 Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana.

18 Bwana ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife.

19 Nifungulieni malango ya haki, Nitaingia na kumshukuru Bwana.

20 Lango hili ni la Bwana, Wenye haki ndio watakaoliingia.

21 Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu.

22 Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

23 Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu.

24 Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.

Zaburi 145:16
16 Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.

Waefeso 3: 20
20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

Zaburi 145: 18 – 19
18 Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.

19 Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.

Zaburi 34: 4
4 Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.

Zaburi. 145: 20
20 Bwana huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza.

Zaburi. 121: 5
5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.

Zaburi 18:2
2 Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.

Zaburi 46:1
1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Yeremia 1:19
19 Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe.
Hitimisho

Zaburi. 124:1 ñ 6
1 Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.

2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.

3 Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.

4 Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.

5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.

6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.

Warumi. 8:37
37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.

×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top