1. Mwombe Mungu akuwezeshe kuisikia na kuitii sauti yake kila anaposema nawe kwa njia mbalimbali
a) Atupe bidii ya kusikiliza sauti yake : Kumb 28 :1, 2.
b) Aondoe uvivu wa kumsikia : Ebr 5 : 11
c) Aondoe uzito moyoni wa kumsikia : Matendo 28 : 27
d) Atupe kuelewa akilini. Math 13:14 -16
e) Atupe ufahamu wa moyoni : Mdo 27:28
2. Msihi Roho Mtakatifu aseme nasi/ kanisa lake kama ilivyokuwa katika kanisa la kwanza la mitume katika kitabu cha Matendo
a) Aseme nasi: Matendo 13:1-2
b) Atuongeze kwenye kweli : Yoh 16: 13
c) Atufundishe na kutukumbusha : Yoh 14:26
3. Jiombee ili uweze kutenga muda wa kuwa na utulivu na Mungu na kukua katika kumjua Yeye.
a) Kutenga muda wa utulivu: Luka 5:15-16, Luka 6:12
b) Ufunuo wa kumjua zaidi : Efeso : 1: 17
4. Ombea viongozi wa kanisa kuanzia ngazi ya taifa, kanisa la mahali pamoja wajae hekima ya Mungu, wawe makini katika kusikia, kuitii sauti ya Mungu, na wasiwe watu wa kuzitegemea akili zao wenyewe.
a) Watende kazi katika hekima ya Mungu. 1 kor 2:4-5
b) Kutembea katika uweza na nguvu za Roho Mtakatifu
c) Kumtegemegea Mungu: Mithali 3:5-6