1. (a) Ombea jambo ama hitaji lolote ambalo unahisi hujaliombea au hatujaliombea na ungependa liombewe – Mathayo 7:7-8
(b) Omba kwa ajili ya ibada zote 3 za Jumapili kesho kwamba Mungu ahudumie watu wake na wafurahie kuwa nyumbani mwa Bwana – Zaburi 122:1
2. Omba kwa kuweka nadhiri mbele za Mungu ya kuwa:
(a) Utampenda na utamtumikia kwa moyo wako wote na kuyaishi maisha matakatifu na ya kumpendeza nyakati zote – Joshua 24:14-18
(b) Utakuwa mwaminifu katika kumtolea sadaka, zaka, na michango mingine kwa ajili ya kazi yake – DPC & PAGT – Genesis 28:20-22
3. Omba kwa kukiri kwamba mambo yote tuliyoyaomba tangu tarehe 6 Januari 2025 mpaka leo tayari yametimia kwa imani katika ulimwengu wa roho na tutayaona yakitokea katika ulimwengu wa kawaida – Marko 11:24-26
4. Mshukuru na kumtukuza Mungu kwa kutupa afya njema, shauku, muda, nguvu, na neema ya kushiriki haya maombi. Shukuru ukiamini kuwa Mungu anatenda sawasawa na tulivyoomba – 1Yohana 5:14-15