MAMBO YA KUOMBEA: JUMAMOSI 23 JANUARI 2021

WIKI MBILI ZA KUFUNGA NA KUOMBA: DPC
11-23 Januari 2021

  1. Mtolee Mungu dhabihu ya sifa. Msifu na kumuabudu Mungu kwa uaminifu wake, wema wake, ukuu wake n.k
    Waebrania 13:15, Zaburi 103:1-5; 95
  2. Tunapokea kwa imani kile tunachoomba, kwahiyo mshukuru Mungu kwa ajili ya kila kitu ulichokiombea. 1 Yohana 5: 14-15, Isaya 65:24, Luka 11: 10-15

• Mshukuru Mungu kwamba kwa Neema yake utatembea katika njia za Bwana, utakuwa na ushirika naye wa kudumu, utampenda kwa moyo wako wote, na kumtumikia yeye peke yake. Yoshua 24:15, Yohana 15: 4-8

• Mshukuru Mungu kwa mambo mapya atakayoyafanya maishani mwako mwaka huu. Mshukuru Mungu kwa sababu mapenzi yake kwako mwaka huu yatatimizwa. Zaburi 138: 8, Ayubu 42:2

• Kwa imani mshukuru Mungu kwa kujibu maombi yako kwa sababu atatimiza ahadi zake kwako. Zaburi 145:18-19; 37: 4

• Mshukuru Mungu kwa upako wa Roho Mtakatifu juu ya maisha yako ambao utakusaidia kutimiza kusudi la Mungu. Matendo 1: 8, Luka 4: 18-19

• Mshukuru Mungu kwa upaji. Mshukuru kwa ajili ya nguvu ya kiungu ambayo itakusaidia kufanya kazi na kufanya mambo zaidi ya uwezo wa kibinadamu. Mshukuru Mungu kwa sababu hutapungukiwa chochote unapojitiisha chini yake kama Bwana. Kumbukumbu 8:18, Wafilipi 4: 18-19, Zaburi 23:1

• Mshukuru Mungu kwa ajili ya baraka ambazo ameachilia katika maisha yako, familia yako, juu ya DPC na juu ya taifa letu.
Zaburi 113: 1-4

• Mshukuru Mungu kwa ulinzi na ushindi ulionao kupitia Yesu Kristo. Mshukuru Mungu kwamba mwaka huu utafanikiwa katika kila eneo la maisha yako. Tangaza kwamba hakuna silaha itakayofanikiwa juu yako na kwamba Mungu atakushibisha kwa uwingi wa siku (atakupa maisha marefu). Zaburi 91:16; 121:1-8, Isaya 54:17, 2 Wathesalonike 3: 3

  1. Kiri na utangaze Zaburi 23.
    ¹Bwana ndiye mchungaji wangu; Sitapungukiwa na kitu.
    ² Katika malisho ya majani mabichi hunilaza kando ya maji ya utulivu huniongoza.
    ³ Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
    ⁴Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
    5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
    6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele. (SUV)

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top