MAMBO YA KUOMBEA: JUMATATU 11/1/2021

WIKI MBILI ZA KUFUNGA NA KUOMBA: DPC
11- 23 Januari 2021

MAMBO YA KUOMBEA: JUMATATU: 11/1/2021

  1. Mshukuru Mungu kwa uaminifu wake katika mwaka 2020. Mshukuru kwa Kumsifu na kumuabudu na maombi; kwa ajili ya neema yake, kibali, upaji, ulinzi na mambo yote ambayo ameyafanya maishani mwako. Zaburi 28: 7; 100: 4-5; 107: 8-9, 1 Wakorintho1: 4
  2. Jiweke wakfu kwa Bwana na kabidhi siku zote za maombi na kufunga. Yoshua 3: 5
    •Omba Roho Mtakatifu atusaidie katika maombi yetu ili tuweze kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Warumi 8:26-27
    •Omba udhihirisho wa nguvu za Mungu kila siku tunapomtafuta. Matendo 4:31
  3. Omba kinyume na pepo wachafu na nguvu za giza zilizojipanga kukuzuia kuomba kwa ufanisi. Omba kinyume na roho za magonjwa, uzito na vitu vyote vinavyoweza kusababisha usumbufu.
    Mathayo 18: 18-19, 1 Petro 5: 8-9.
  4. Mshukuru Mungu kwa ajili ya upako na uhuru wa kuomba. Mshukuru Mungu kwa udhihirisho wa utukufu wake katikati yetu tunapoutafuta uso wake.
    2 Wakorintho 3: 17-18

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top