MAOMBI YA IJUMAA 17/7/2020.

WIKI MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA DPC
13-18 JULAI 2020

MAOMBI YA IJUMAA 17/7/2020.

Mathayo 6:13a …. Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule mwovu.

  1. Omba kwamba uzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Waefeso 6:10. Omba uvishwe silaha zote za Mungu.
    Waefeso 6:13-18. Omba kwamba uendelee kuwa na ushirika na Mungu, udumu katika neno lake, ukue katika imani, na uwe hodari katika maombi. Mathayo 7:24-27, Yohana 15:7
  2. Omba kwamba Mungu atakulinda na kila mtego na mashambulizi ya shetani ambae ni kama simba angurumaye .
    1 Petro 5:8, Zaburi 121:7-8, Yohana 17:15, 1 Nyakati 4:10. Omba Mungu ainuke na adui zake ambao ni adui zako watawanyike.
    Zaburi 68:1-3. Amuru kila mlima kwenye maisha yako uhame kwa jina la Yesu. Marko 11:23-24
  3. Omba ulinzi wa Mungu juu ya maisha yako, familia yako na Kanisa.
    1 Yohana 5:18-19. Tangaza kwamba kila silaha itakayoinuka juu yako haitafanikiwa. Omba Zaburi 91.
  4. Mshukuru Mungu kwa ajili ya mamlaka uliyonayo katika Kristo Yesu. Mshukuru kwa sababu unashinda na zaidi ya kushinda katika Kristo Yesu.
    1 Wakorintho 15:57, 1 Yohana 4:4, Warumi 8:3

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top