MAOMBI YA JUMAMOSI 18/7/2020.

WIKI MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA DPC
13-18 JULAI 2020

MAOMBI YA JUMAMOSI 18/7/2020.

Mathayo 6:13b Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina

  1. Msifu na kumuabudu Mungu kwa maana Ufalme na nguvu na utukufu ni vyake. Msifu na kumuabudu kwa ajili ya ukuu wake, uaminifu wake katika kutimiza ahadi zake.
    Isaya 44:6, 1 Nyakati 29:11, Ufunuo 5:12
  2. Omba Roho Mtakatifu akujaze nguvu kulitumikia kusudi la Mungu. Matendo 1:8, Isaya 40:29-31. Omba Roho Mtakatifu akupe nguvu, hekima, maarifa na ufahamu. Isaya 11:2. Omba kwamba uweza wake wa Uungu utakukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa. 2 Petro 1:3-4
  3. Mshukuru Mungu kwa kila jambo uliloliombea kwa sababu anajibu maombi. 1 Yohana 5:14-15
  4. Kiri Zaburi 23
    1 BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU SITAPUNGUKIWA NA KITU.
  • Asante Bwana kwa kuwa Mchungaji Mwema kwangu. Nitakutii siku zote, na hivyo sitapungukiwa na chochote.

2 KATIKA MALISHO YA MAJANI MABICHI HUNILAZA, KANDO YA MAJI YA UTULIVU HUNIONGOZA.

  • Asante Bwana kwa kunipa mahitaji yangu. Natangaza kwamba ninapoenenda katika njia zako nitafanikiwa katika kila nilifanyalo.

3 HUNIHUISHA NAFSI YANGU; HUNIONGOZA KATIKA NJIA ZA HAKI KWA AJILI YA JINA LAKE.

  • Asante Bwana kwa ajili ya Roho wako Mtakatifu anayeniongoza kuyafanya mapenzi yako. Natangaza kwamba maisha yangu yatakupa heshima.

4 NAAM, NIJAPOPITA KATI YA BONDE LA UVULI WA MAUTI SITAOGOPA MABAYA; MAANA WEWE UPO NAMI, GONGO LAKO NA FIMBO YAKO VYANIFARIJI.

  • Nakushukuru Bwana kwa ulinzi na mkono wako juu ya maisha yangu. Natangaza kwamba sitaogopa mabaya kwa maana chini ya mbawa zako niko salama.

5 WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU, UMENIPAKA MAFUTA KICHWANI, KIKOMBE CHANGU KINAFURIKA.

  • Nakushukuru Bwana kwa ushindi nilionao katika Kristo Yesu. Natangaza kwamba mimi ni mshindi na zaidi ya kushinda kwa Kristo Yesu na nitasherehekea ushindi wangu mbele ya watesi wangu kwa utukufu wako.
  • Nakushukuru Bwana kwa ajili ya nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha yangu, natangaza kwamba nimepakwa mafuta kulitumikia kusudi la Mungu na kikombe changu kinafurika.

6 HAKIKA WEMA NA FADHILI ZITANIFUATA SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU; NA NITAKAA NYUMBANI MWA BWANA MILELE .

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top