MAOMBI YA JUMANNE 14/7/2020

WIKI MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA DPC
13-18 JULAI 2020

MAOMBI YA JUMANNE 14/7/2020
Mathew 6:10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.

  1. Omba kubadilishwa kwa nia na moyo wako ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu. Warumi 12:2. Omba ujazwe maarifa ya mapenzi ya Mungu katika hekima yote. Wakolosai 1:19, Zaburi 143:10
  2. Omba mapenzi ya Mungu yatimizwe katika maisha yako, familia yako, na Kanisa nk. Omba kwamba chochote ambacho Mungu amekusudia kufanya kwenye maisha yako katika msimu huu kitatimia. Isaya 14:27, Yeremia 29:11-12,
  3. Omba kinyume na roho za kipepo zilizojipanga kukuzuia kuyafanya mapenzi ya Mungu na kutembea katika ushindi wako. Yakobo 4:7, Mathayo 4:3-11
  4. Ombea uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020. Omba Mungu ainue viongozi wenye hofu ya Mungu watakaoyafanya mapenzi yake. Omba tupate viongozi ambao mioyo yao ni kwa ajili ya watu na taifa. Omba kusudi la Mungu lisimame Tanzania. Mithali 19:21

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top