MAOMBI YA JUMATATU 13/7/2020

WIKI MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA- DPC.
13-18 JULAI 2020

MAOMBI YA JUMATATU 13/7/2020

Mathayo 6:9 Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.

  1. Msifu na kumuabudu Mungu na ulitukuze jina lake kwa mambo makubwa aliyoyafanya na anayoendelea kufanya katika maisha yako. Zaburi 145:1-5, 86:12, 95:1-6.
  2. Mshukuru Mungu kwa wema wake, uaminifu wake na kwa kila jambo alilokutendea tokea Januari mpaka sasa. Zaburi 103:1-5
  3. Omba Roho Mtakatifu aliye msaidizi wetu akuwezeshe kuomba sawa sawa na mapenzi ya Baba. Omba roho ya neema na maombi. Zakaria 12:10, Warumi 8:26
  4. Omba udhihirisho wa nguvu za Roho Mtakatifu tunapomtafuta katika maombi. Yeremia 33:3, Waefeso 3:20, 1 Wakorintho 2:9-10

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top