MAOMBI YA JUMATANO 15/7/2020.

WIKI MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA DPC
13-18 JULAI 2020

MAOMBI YA JUMATANO 15/7/2020.

Mathayo 6:11 Utupe leo mkate wetu wa kila siku.

  1. Omba Roho Mtakatifu akusaidie kuyafanya mapenzi ya Mungu, kutembea katika njia zake na kuwa shahidi na wakili mwaminifu wa kile Mungu alichokupa. Mathayo 6:32-33. Omba moyo wa kutoa kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. 2 Wakorintho 9:7-9, Wafilipi 4:19
  2. Peleka haja zako mbele za Mungu na omba baraka zake kukufanikisha na kukupa hekima, maarifa na ufahamu wa kiungu utokao juu. Mithali 10:22, Kumbukumbu 8:18-19
  3. Omba baraka za Mungu kuachilia nguvu na kibali cha kiungu kitakachokusababisha kukua na kuongezeka katika lolote ufanyalo. Omba Mungu azibariki kazi za mikono yako.1 Nyakati 4:10, Zaburi 90:17
  4. Ombea maono na mipango ya DPC. Omba Mungu alibariki kanisa kwa pesa na rasilimali nyingine ili kutimiza azma zake. Ombea kila mshirika kutoa kwa uaminifu kwa ajili ya kazi ya Bwana DPC. Wafilipi 1:6, 4:19, 2 Wakorintho 8:1-7
  5. Ombea mafanikio ya taifa lako. Yeremia 29:7. Ombea ukuaji wa uchumi wa taifa la Tanzania ili liweze kuwa baraka kwa mataifa mengine. Ombea viongozi na wote wenye mamlaka Mungu awape hekima na maarifa kutawala na kukuza uchumi kama Mungu atakavyo. Mithali 16:16, 1Wafalme 4:29-31, 2 Nyakati 1:10

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top