PARENTING SEMINAR (SEMINA YA MALEZI)

Semina Ya Malezi


•MUKTADHA WA MJADALA WETU

NENO LA MUNGU- YAANI BIBLIA

UTANGULIZI:

•MALEZI YANAYOFAA HUANZA NA MUNGU

•Mwanzilishi wa uhai, ndoa na familia

•HUWEZI KUONGELEA MALEZI BILA KUONGELEA MAHALI YANAPOFANYIKA!

•MWANZO 1:26-28 –Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. Na kuitiisha…” 

•Utaratibu wa Mungu ni kuwa kila mtoto azaliwe ndani ya familiaya baba na mama

•Mungu ndiye mwanzilishi wa taasisi ya familia: Baba, Mama, Mtoto/Watoto

•MAZINGIRA FULANI YASIYOKWEPEKA HUWEZA KUSABABISHA MZAZI MMOJA ASIWEPO

TUNGEZINGATIA 1Tim 5:8  na 1Yoh.4:20-21- WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU WANGEKUWA WACHACHE SANA

•Watoto kuzaliwa nje ya ndoa ni matokeo ya anguko na kuhalifu sheria ya Mungu; Kutoka 20:14

•Watoto toka kaya za wazazi walioachana pia ni matokeo ya angukoWaefeso 5:25

•Watoto wa jinsi hii hawana kosa lolote au dhambi ila hubebeshwaisivyostahiki lawama ya matendo ya wazazi wao- ‘mwanaharamu’ 

•Mara nyingi hupata shida mbalimbali za malezi na makuzi ILA mbeleza Mungu, Watoto hawa wana haki sawa na waliozaliwa kwenyendoa.

MALENGO YA MSINGI YAMALEZI:

1.KUZALISHA ‘NATURE’(hulka, maumbile, desturi, mazoea,jinsi, namna)  YA MZAZI NDANI YA MTOTO :

  Hulka Ya Mungu Kupitia Wazazi Kwenda Kwa Mtoto

2.KUZALISHA ’CHARACTER’ (TABIA/MWENENDO) WA MZAZI NDANI YA MTOTO

  Maadili ya ki-Mungu Kupitia Mzazi Kwenda kwa Mtoto

3.KUZALISHA  ‘BEHAVIOR’ (MWENENDO/SILKA) YA MZAZI NDANI YA MTOTO

  Mungu alituumba tufanane naye katika kuwaza kwetu, tabia zetu na

   matendo yetu

•MAZINGIRA

•MAZINGIRA YA SASA YANA UGUMU SANA KWA WAZAZI KULEA SABABU YA:

•MUINGILIANO WA DUNIA NA TEKINOLOJIA

•Watoto kwa vijana kushawishika kwenye vitendo vya kuangaliapicha za ngono, kamari, picha za uchi, nyimbo zenye maudhui yakujiua, utukuzaji wa Maisha ya makundi ya mtaani ya kihalifu(ganster lifestyle); kuiga mitindo ya Maisha ya wengine namengine mengi

•MMOMONYOKO WA DESTURI ZA MAISHA YA KIFAMILIA KIBIBLIA

  (The Collapse of traditional Biblical family Lifestyles)

•Familia Ni Nini?

•Maana tofauti kwa watu tofauti

•Hutegemea jamii husika

•Mara nyingine hutegemea kiwango cha maendeleo ya kiuchumi

•Unit ndogo zaidi ya jamii yoyote

•Kiwanda cha kutengeneza jamii

•Chanzo

•TAASISI ILIYOANZISHWA NA MUNGU MWENYEWE!  

•Mwanzo 1:26: “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale….” agizo, mamlaka, uwakili (mandate)!

•27: “…mwanaume na mwanamke aliwaumba…zaeni,mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale…”

•Mwanzo 2:18 “Si vema…nitamfanyia msaidizi wa kufanananaye”

•23:… mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyamayangu…

•24:… mwanamume atamwacha….ataambatana na mkewe…mwili mmoja”

•Mifumo ya Uanzishwaji wA Familia

•Karne za mwanzo:  

•Mwanzo 24:1-67 Ibrahim akimuapisha mtumishi wake asimtwalie mwanae Isaka mke ktk binti za Wakanaani- bali ktknchi yake kwa jamaa zake! Akampata Rebeca; 

•Mwanzo 29: 10-20- hadithi ya Yakobo na Raheli

•Karne ya 18 Courtship began

•WWII- Less concerned on a man’s status and more with his survival

•Karne ya 21: 

•GOING ON A DATE, DATING, COURTSHIP AND MARRIAGE

•Cyberdating

•Matarajio ya wanandoa watarajiwa- yamebadilika?

•Maandalizi ya Ndoa

•Nini ni vipaumbele?

•Afya za wahusika

•Mgawanyo wa majukumu

•Majukumu ya Ki-familia

•Nyakati za Agano la Kale na Agano Jipya

•Mwanzoni mwa Karne ya 19

•Mwishoni mwa Karne ya 19- Vita ya kwanza ya Dunia…halafumapinduzi ya viwanda- mabadiliko na mageuzi kwenyemajukumu ya kina mama

•Majukumu ya Wazazi Kifamilia- Tanzania ya karne ya 21

JE, KUNA TOFAUTI?

•Familia za vijijini

•Familia za mjini

•Familia za ‘wasomi’

•Maendeleo ya Kiuchumi na Familia

•Kazi kutofanyika kifamilia- ulimwengu wa ajira

Wanawake kuwa na uwezo kiuchumi- BARAKA/CHANGAMOTO KWENYE NDOA

•Majukumu ya baba yamebadilika?

•Majukumu ya Mama yamebadilika?

•Ukasimishaji wa majukumu

•Mabadiliko ya Jamii na Matokeo kwa Familia

•Wanafamilia/ukoo kuishi mbalimbali

•Mtazamo finyu wa familia ni nini/nani na athari zake(accountability)

•‘Mzoroto’ wa uanzishwaji wa asasi za kushughulika na masualaya kijamii yaliyobebwa na familia hapo awali

•Mitazamo tofauti ya malezi

•Urahisi wa kuachana

•Maendeleo ya Tekinolojia na Familia

•Utandawazi- elimu, taarifa, kuigana

Usasa na Ushamba– athari kwa Watoto na Wazazi

•Uelewa finyu wa tekinolojia inavyofanya kazi

•Ukosefu wa Maisha ya faragha

•Hisia za kutoaminiana wanandoa- MIGOGORO/UVUNJIFU WA NDOA

Maendeleo yaTekinolojia na Familia

KELELE NYINGI! TUMSIKILIZE NANI?

•NINI KIFANYIKE

•Turudi kwenye misingi -2Timotheo 3:16; 1Timotheo 4:11-16

•Tujielimishe- Elimu Haina Mwisho   Mithali 4:13

•Tujaliane-1Timotheo 5:8 

•Malezi na Makuzi

•MITHALI 22:6; KUMB.6:1-12; EMPHASIS VS 1-5, 6-9

•MAHITAJI MUHIMU: CHAKULA, MAVAZI, MALAZI, ELIMU

•KUJISIKIA SALAMA

•UPENDO

•HESHIMA

KUJITAMBUA: AFYA YA MWILI, NAFSI NA ROHO

UWAJIBIKAJI

•Malezi na Makuzi: CHAKULA

MAANDALIZI KABLA MIMBA HAIJATUNGWA NA WAKATI WA UJAUZITO:

LISHE: LISHE YENYE UWIANO NI MUHIMU WAKATI WOTE. ILA KWA MJAMZITO NI MUHIMU ZAIDI. ILI MTOTO AKUE VIZURI TUMBONI ANAHITAJI:

FOLIC ACID- A ‘B’ VITAMIN- CAN HELP PREVENT BIRTH DEFECTS OF THE BRAIN AND SPINE (NTD); HEART DEFECTS, DEFECTS IN YOUR BABY’S MOUTH (CLEFT LIP AND PALATE):

CHAKULA: Citrus fruits, Green leafy vegs,Beans…enrichedfoods:cereals,bread,

IRON (MADINI YA CHUMA): Hutengeneza hemoglobin- Protini inayosafirisha oxygen toka kwenye mapafu kwendakila sehemu ya mwili.x2! Inatengeneza damu:

CHAKULA: Nyama nyekundu, nyeupe, viumbe bahari, mbogaza majani za kijani,maharage, njugu, zabibu kavu na matundayaliyokaushwa

Vyakula vyenye vitamin C husaidia mwili kupokea madini yachuma yaani Iron- machungwanyanyamadalanzi n.; kilasiku

Calcium itokanayo na Wanyama kama maziwa, kahawa, chai, kiini cha yai, chakula chenye fiber na soya huzuia upokeaji waIron kwenye mwili! EPUKA HIVI ULAPO VYAKULA VYENYE IRON

•Malezi na Makuzi: CHAKULA

IRON:  USIPOPATA IRON YA KUTOSHA KUNA UWEZEKANO WA KUPATA

•INFECTIONS

•ANAEMIA

•UCHOVU

•MTOTO NJITI- KABLA YA MAJUMA 37 YA UJAUZITO

•UZITO MDOGO WA MTOTO

•Malezi na Makuzi: CHAKULA

CALCIUM: Madini yanayosaidia kujenga mifupa na meno, moyo, misuli na neva

VYAKULA: Maziwa fresh, mgando na jibini; broccoli na Kale; Juisi ya machungwa kama imeongezwa calcium

USIPOPATA CALCIUM ya kutosha, mwili wako huifyonza kutoka mifupa yako na kumpelekea mtoto anayetengenezwa tumboni! 

Hii itapelekea kupata athari za kiafya kwa mama kama meno kung’oka AU ‘Osteoporosis’ baadaye sana kwenye maisha. Ugonjwa huu husababisha mifupa kuwa myembamba na kuvunjika kwa urahisi

•Malezi na Makuzi: CHAKULA

VITAMIN D : Husaidia ufyonzwaji wa calcium mwilini

Husaidia utendaji kazi mzuri wa nerves,misuli na mfumo wa kinga ya mwili

Mfumo wa kinga ya mwili husaidia mwili usipate maambukizi

Vitamin D husaidia mifupa na meno ya mtoto kujengeka vizuri

CHAKULA: Samaki wenye mafuta kama salmon; maziwa na nafaka zilizoongezwa kirutubishi hicho

•Malezi na Makuzi: CHAKULA

DHA (Docosahexaenoic Acid): ni aina ya mafuta (Omega-3 fatty acids)

•Husaidia ukuaji na ujengekaji mzuri wa mtoto tumboni- hasa hasa utengenezwaji wa ubongo na macho

Vyakula: vya baharini (visivyo na zebaki) kila wiki: Herring, salmon, trout, anchovies, halibut, catfish, shrimp and tilapia

•Pia atumie: juice ya machungwa, (maziwa, mayai kama yameongezwa DHA).

•Malezi na Makuzi:CHAKULA

IODINE (Madini joto): Ni madini mwili huhitaji kwa ajili ya homoni ya thyroid ambayo husaidia mwili wako kutumia na kutunza nguvu itokanayo na chakula unachokula.

•Husaidia ukuaji mzuri wa mfumo wa neva kwa mtoto( Ubongo, uti wa mgongo na nerves zenyewe)- ambao humsaidia mtoto kujijongeza (move), kufikiri (think)na kuhisi (feel).

VYAKULA: Samaki, maziwa, jibini, yoghurt, chumvi iliyoongezwa madini joto haya na nafaka na mikate iliyoongezwa Iodine

•Malezi na Makuzi: MAVAZI

•YAWE SAHIHI KUENDANA NA UMRI, HALI YA HEWA NA MAHALI UNAPOKWENDA

•MZUNGUMZIE SUALA LA MAVAZI MKIWA NYUMBANI NA MITINDO MBALI MBALI ILI MJIELIMISHE NA KUELIMISHANA

•UWE MFANO WA UVAAJI MZURI NA NADHIFU

•SIFIA PALE MWANAFAMILIA AMEVAA VIZURI ILI KUREINFORCE KILE UNACHOWAFUNDISHA

•KUBALI KUKOSOLEWA NA KUBADILI NGUO UKIAMBIWA HAIFAI 

•Malezi na Makuzi: MALAZI

•IKIWEZEKANA, MTOTO AHAMISHWE CHUMBA CHA WAZAZI AKIFIKISHA MWAKA MMOJA

•TENGANISHA VYUMBA KWA JINSIA- KAMA UNAWEZA, WAFANYAKAZI WASILALE NA WATOTO WAKO HATA KAMA NI WA JINSIA MOJA

•WAGENI TUNAWAPENDA, ILA WASILALE NA WATOTO WETU VYUMBANI- WENGI WAMEFUNZWA TABIA ZISIZOFAA NA NDUGU WA KARIBU

•WATOTO WAFUNDISHWE KULALA NA NGUO PANA ZINAZORUHUSU MWILI KUPUMUA NA HAPO HAPOWAMEJISETIRI

•WATOTO WAFUNDISHWE KUTANDIKA VITANDA VYAO NA KUWEKA VYUMBA KATIKA HALI YA USAFI TANGU WAKIWA WADOGO

•Malezi na Makuzi: ELIMU

•ELIMU HUANZA MTOTO AKIWA MDOGO KABISA: 

•MUONYESHE VITU MBALIMBALI, MFUNZE KILA KITU- KUIMBA, KUPIGA MAKOFI, KUOMBA, KUBEMBELEZA- WATOTO HUIGA 70% YA WANACHOONA

•WATOTO HUJIFUNZA KWA KUANGALIA ZAIDI KINACHOFANYIKA NA KUKIIGA

•UNAPOTAFUTA SHULE HATA YA AWALI- ITEMBELEE UJIRIDHISHE NA MAZINGIRA NA KINACHOENDELEA HAPO

•KAGUA MADAFTARI YA MTOTO NA KUMUULIZA MASWALI ILI UMSAIDIE INAPOBIDI

•NENDA SHULENI MARA KWA MARA KUANGALIA MAENDELEO NA KUMTIA MOYO MTOTO NA ANAPOSHIRIKI MICHEZO NENDA KUMSHANGILIA

•AKITOKA SAFARI ZA MAFUNZO-HATA KWA BABU NA BIBI, KETI NAYE NA KUMUULIZA MASWALI

•Malezi na Makuzi: eLIMU

•ZUNGUMZA NA WATOTO SAFARI YAO YA ELIMU, WANATAKA KUWA NANI NA KUITUMIAJE ELIMU WANAYOPATA- WATIE MOYO NA WASAIDIE MIKAKATI SAHIHI YA KUFIKIA AZMA YAO

•WAKUMBUSHE MARA KWA MARA KUOANISHA WANACHOJIFUNZA NA MAISHA YAO YA KILA SIKU- WAIONE ELIMU KAMA NYENZO YA KUWASAIDIA KUMUDU MAZINGIRA YAO NA SIO KUKARIRI KWA AJILI YA KUSHINDA MITIHANI NA KUAJIRIWA

•WASAIDIE KUFANYA KAZI MAHALI KWA VITENDO WAKATI WA LIKIZO- NI VIZURI ZAIDI WAKIUELEWA ULIMWENGU WA KAZI MAPEMA

•KUJISIKIA SALAMA

•KUTOKA 14:13-14; KUMB.1:29-31; MITHALI 18:10;

•MTOTO ANA HISIA TOKA TUMBONI- EPUKA HASIRA NA MAGOMVI

•HAKIKISHA UNATENGENEZA MAZINGIRA YA AMANI NA MSHIKAMANO NYUMBANI WAKATI WOTE ILI WATOTO WAJISIKIE SALAMA NA KUPAPENDA NYUMBANI

WASIKILIZE SANA WATOTO NA WAPE NAFASI YA KUJIELEZA BILA KUHUKUMU

•KUJISIKIA SALAMA

•WAJULISHE KUWA MUNGU AMEWAPA NINYI WAZAZI KAZI YA KUWALINDA NA WASIOGOPE KUKWAMBIA CHOCHOTE- JENGA URAFIKI

•WAFUNDISHE NA KUWAKUMBUSHA WATOTO KUWA YUPO MUNGU ANAYEWATETEA KATIKA YOTE- SOMA NAO NENO ILI WAJIFUNZE KUMTEGEMEA MUNGU

•WAFAHAMU MARAFIKI ZA WATOTO WAKO VIZURI, IKIBIDI NA FAMILIA WANAZOTOKA

•FAHAMU NYENDO ZA WATOTO WAKO WAKATI WOTE NA WAFUNDISHE TAHADHARI ZA KIUSALAMA

•UPENDO

•KWANZA WAFUNDISHE WATOTO UPENDO WA MUNGU KUPITIA VITU WANAVYOVIONA

•WAONYESHE WALIVYOPENDELEWA NA MUNGU KUPITIA MIFANO KADHA WA KADHA KATIKA JAMII

•WAAMBIE KUWA UNAWAPENDA BILA MASHARTI NA WAONYESHE KWA VITENDO

•UNAWACHANGANYA WATOTO UNAPOWAAMBIA UNAWAPENDA NA HAPO HAPO UNAMCHUKIA,

    UNAMSEMA VIBAYA, UNAMTUKANA AU KUGOMBANA NA MTU MWINGINE WANAYEMPENDA SANA-

    BABA AU MAMA

•USIHAMISHIE UGOMVI WENU KWA WATOTO- WANAUMIA ZAIDI KULIKO WEWE MZAZI NA KUJISIKIA SI   

    SALAMA

•HESHIMA

KUTOKA 20:12; WARUMI 13:1-7; WAEBRANIA 13:171PETRO2:17

•HESHIMA HUANZA KWA MTU KUJIHESHIMU MWENYEWE- WAFUNDISHE KUJUA THAMANI YAO

•JINSI YA KUDHIHIRISHA HESHIMA HUTOFAUTIANA KUTOKA JAMII MOJA HADI NYINGINE- SOMA MAZINGIRA ULIYOPO NA USIWAKWAZE

•JIFUNZE KUHESHIMU WATU WENGINE NA WAFUNDISHE WATOTO KWA VITENDO

•KUJITAMBUA

•HILI NI ENEO LENYE UTATA SANA KWA SABABU YA CHANGAMOTO ZA UTANDAWAZI NA KUIGANA

•JAMBO LA MSINGI WAJITAMBUE WAO NI NANI 1PETRO 2: 9

•MAWASILIANO

•MAWASILIANO NI KATI YA WATU WAWILI AU ZAIDI- PENDA KUSIKILIZA ZAIDI KUJUA ULIMWENGU WA MWANAO

•KILA MTU HUPOKEA TOFAUTI- JIFUNZE NAMNA YA MTOTO WAKO

•WASILIANA NA MTOTO KUTEGEMEA RIKA LAKE

•ANGALIA MAZINGIRA ULIYOPO NA UNACHOWASILIANA NAYE

•TUMIA MANENO SAHIHI YA KUTOA MWONGOZO SIO HUKUMU UNAPOWASILIANA NA MWANAO

•UWAJIBIKAJI

•WAFUNDISHE WATOTO KUWAJIBIKA KUTEGEMEA UMRI WAO

•WATOTO WASIKAE BURE NYUMBANI BALI WAJITEGEMEE

•TENGENEZA MAZINGIRA YA WAO KUWAJIBIKA KWA:

•MUDA WAO

•KWENYE FAMILIA

•KWENYE JAMII ILIYOWAZUNGUKA

•KANISANI

•SHULENI

•WAKUMBUSHE KUPITIA NENO LA MUNGU KUHUSU KUWAJIBIKA NA WASIWE NA UTUMWA WA MACHO Wakolosai 3: 18-25a

• Wafinyanzi wa mtoto

• NENO LA MUNGU:KUMB.6:7-9

•NAFASI YA BABA

•NAFASI YA MAMA

•NAFASI YA KANISA KAMA SEHEMU YA JAMII: kufundishaInjili kamili, kukemea

•NAFASI YA JAMII PANA: TUFIKE MAHALI TUWEKE MIFUMO YA KULEA PAMOJA

•TUKUBALI WATOTO WETU KUKOSOLEWA NA WATU WENGINE

•NAFASI YA TAASISI: SHULE NA SHERIA ZAKE;  MITAALA

BADO KUNA TUMAINI.

HUJACHELEWA! HATA KAMA KUNA MAHALI ULITELEZA WAWEZA KUREKEBISHA!

MUNGU NI WA REHEMA NYINGI!

•Rejea zilizotumika

Biblia Takatifu, The Bible Society of Tanzania and The Bible Society of Kenya, United Bible Societies, 1952

Myles Munroe & David Burrows 2007. Kingdom Parenting: Raising great kids in a changing world; Religious Broadcasting Books Publishers

Psychology Today Website- 7 Rules for Parents to Improve Your Child’s Future

ASANTENI KUNISIKILIZA.

MUNGU AWABARIKI SANA NA KUWAWEZESHA KULEA VIZURI

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top