JAZA CHOMBO CHAKO

UJUMBE: JAZA CHOMBO CHAKO. KIFUNGU: YOHANA 2:1-11

FUNZO #1 UWAJIBIKAJI [CHUKUA MAJUKUMU}
[MWANZO 2:15]

FUNZO #2 AMINI NA KUMTUMAINI MUNGU
YOHANA 11:38-44

YOHANA 2:1-11 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5 Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. 6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. 8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.

9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, 10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

MWANZO 2:15
15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.

YOHANA 11:38-44
38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?

41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.

44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top