TUNAENDELEA KULITUMAINI JINA LA BWANA, MUNGU WETU

TUNAENDELEA KULITUMAINI JINA LA BWANA,MUNGU WETU

KITABU
ZABURI 20:1-9 Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote.

Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama. Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.

-Kutumaini au umuamini mtu au kitu si jambo jepesi kutokea

-Lazima pawepo na sababu za msingi ili tendo la kutumaini/kuamini/kuaminiana litokea

-Kuamini au kutumaini inahitaji upande mmoja au pande zote kuthibitisha uaminifu,uadilifu,imani,uhakika,uwezo,nguvu

-Kijamii- kuaminika ni katiya tabia za msingi mtu muadilifu au kiongozi kuwa nazo.

-Kuaminika inabaki kuwa kigezo muhimu kinachohitajika katika uendeshajiwa mashirika na taasisi nyingi.

-Katika Agano la kale neno kuaminikia liliitwa batah- likimaanisha hali ya kuwa na usalama unaotoka kwa mtu au kiti chenye uhakika na uwezo.

-Neno hili huweza kutumiwa katika mtazamo chanya au hasi.

ZABURI 4:5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana.

ZABURI 41:9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.
MITHALI 28:26 Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.

2 TIMOTHEO 2:13 Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

I. KUPITIA JINA BWANA MUNGU WETU TUNAPOKEA WOKOVU

[MATENDO 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
WARUMI 10:12-13 Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.]

II. KUPITIA JINA LA BWANA MUNGU WETU TUNASAIDIWA SHIDA ZETU

ZABURI 116:1-7 Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa. Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa Bwana amekutendea ukarimu.

ZABURI 50:15 Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.

×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top