Siku 21 za Kufunga na Kuomba. (15 Januari 2024) Umoja, Heshima na Utii

UMOJA, HESHIMA NA UTII.

DAR ES SALAAM PENTECOSTAL CHURCH
Siku 21 za Kufunga na Kuomba. (15 Januari 2024) Siku ya 8
UMOJA, HESHIMA NA UTII. 1 Yohana 4:20-21;  Yohana 13:35; 2 Mambo ya Nyakati 30:12

  1. Uwe na roho ya upendo kwa Mungu, kwa watu wengine, kwa viongozi wa kanisa na serikali.
     Warumi 12:16-18; 13:1-7; 2 Mambo ya Nyakati 30:12

    Tuombe kwa ajili ya Upendo wa ndugu ndani ya kanisa na familia zetu. 1 Yohana 4:12
    Kuwaheshimu watu wengine na kuwajali maana wote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. 
  2. Umoja katika kanisa la DPC1 Wakorintho 1:10; 3:1-3; 12:12-13, Waefeso 4:3,16
    – Omba kila mmoja asimame katika nafasi yake. Warumi 12:4-5
    – Ombea karama mbalimbali ndani ya kanisa. Waefeso 4:11-13 
  3. Umoja katika Makanisa ya PAG na mwili wa KristoWaefeso 4:3,16; 
    –  
    Ombea Umoja kuanzia ngazi Kanisa hadi juu katika kanisa la PAG Tanzania.
    – Maana sisi zote tunategemeana tu viungo katika mwili kujenga kanisa imara. Zaburi 133:1
  4. Ombea Amani kwenye mataifa ambayo yamekubwa na machafuko, Vita na majanga mbalimbali.
    – Mungu wa amani ashushe amani mashariki ya kati, Taifa la Israeli na Mataifa mengine dunianikote.
    – Omba kwa ajili ya nchi ambazo wakristo hawana uhuru wa kuabudu ili Mungu aguse mioyo ya viongozi wa nchi hizo.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top