SIKU YA 16 – SIKU 21 YA KUFUNGA NA KUOMBA

Maombi ya siku 21, Wiki ya TATU

Siku ya 16, Tarehe 24 January 2023. Ombi Kuu; UCHUMI 

1. Ombea uchumi wako, uchumi wa familia yako. 

– Mungu akufunulie fursa ya KAZI, BIASHARA, KUJIAJIRI, iliyo mbele yako. Wafilipi 4:19 Mhubiri 11:4-6

– Kazi ya mikono ibarikiwe. Zab 90;17

– Mungu akupe moyo wa uwakili kwa ajili ya kanisa katika utoaji. Kumb. 8:18. 1Wathes. 4:11-12. Isaya 48:17.   

2. Ombea uchumi wa makanisa ya PAG Tanzania kutoka ngazi ya Kanisa (DPC) hadi Taifa na idara zake zote. 2 Wakorintho 8:9.

a. Ombea Makanisa yawe na maeneo mengi ya kujenga majengo ya Ibada na ya huduma za Jamii. 

b. Mungu awabariki wachungaji wa makanisa yote (DPC-TAIFA).

3. Ombea uchumi wa Taifa la Tanzania kwa ujumla kutoka ngazi ya chini hadi juu. 

– Rasilimali zitumike vyema.  

– Uaminifu kwa kila kiongozi kwa ngazi zote.

– Tuwaheshimu Viongozi wetu wa ngazi zote. 1Petro 2;17

– Omba kinyume na roho za RUSHWA, USHIRIKINA, USUMBUFU KWA WANAAOMBA KAZI, Kut 23:8, Kumb 10:17, Mhubiri 7:7

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top