SIKU YA 20 – SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA

JUMAMOSI 28 JANUARI 2023

SHUKRANI NA MAHITAJI BINAFSI

1. Mshukururu Mungu atendaye mambo makubwa kwa wale wamwitao kwa roho ya unyenyekevu Luka 17:11-19;  Waefeso 3:20 – 21; Zaburi 107:1 – 9

• Mshukuru Mungu kwa uzima, afya njema, ulinzi, mafanikio.

• Mshukuru Mungu kwa neema ya wokovu Efeso 2:8 – 9

• Mshukuru Mungu kwa familia aliyokupa, na kwamba amewalinda na kuwatunza – wazazi, mwenza, Watoto, ndugu.

• Mshukuru Mungu kwa kuwa mpaji wako Zaburi 132:15

2. Ombea mahitaji yako binafsi, familia yako kadri Roho Mtakatifu atakavyokuongoza Isaya 1:18 Wafilipi 4:6; 1 Yohana 5:14 – 15

Ombea mahitaji ya kiroho – Omba Mungu akusaidie kukua kiroho, uaminifu kwa Mungu, kwa kanisa na katika kumtumikia.

• Ombea mahitaji yako ya kimwili – Omba Mungu akupe uzima, afya njema, ulinzi, mafanikio

• Omba Mungu afanikishe malengo na mipango yako

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top