SIKU YA KWANZA – SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA

SIKU YA KWANZA

1. Kujiweka wakfu na kujitakasa kwa Bwana kwa ajili ya Maombi haya kuanzia leo hadi mwisho. Warumi 12:1

 – Kuomba Rehema za Mungu. Zab 51:1

 – Mungu atujalie Roho ya Maombi. Zekaria 12:10a

 – Roho Mtakatifu atusaidie na kututia Nguvu katika maombi haya.  Warumi 8:26

2. Kumshukuru Mungu kwa alivyotusaidia hadi sasa na kwa neema yake ametukirimia mwaka mpya .

 – Ametuvusha katika maeneo mengi. Maombolezo 3:22. Zab 118:21

 – Mshukuru Mungu kwa ajili ya Kanisa la Mahali “DPC” na makanisa yote ya Pentecostal Assmblies of God Tanzania na makanisa mengine ndani na nje ya Tanzania. Zab 136:1-10

 – Mshukuru Mungu kwa ajili Taifa letu la Tanzania na uongozi wake.  1 Timotheo 2:1. 1 

3. Tuyakabidhi maombi yote yatakayoombwa hapa mbele za Mungu. 

 – Mwombe Mungu kwa ajili ya maombi mapya na utakayomkumbusha.…Isaya 43:26

 – Tuwakumbuke washirika wote waweze kuja kumwomba Mungu. Waefeso 1:16 

4. Omba kwa ajili ya watumishi wote wa DPC na PAGT, Mungu awawezeshe kutimiza kusudi lake.     Wakolosai 3;23

 – Wachungaji wote

 – wakalimani wote

 – Team za  Kusifu na Kuabudu

 – Team nzima za media 

 – Team za wahudumu wote

 – Walinzi wote. 

 – Na wengineo ambao hawajatajwa hapa.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top