MAOMBI YA KUFUNGA- SIKU YA SITA- 9 JULAI, 2022

Dar Es Salaam Pentecostal Church (DPC)

Maombi ya Kufunga na kuomba  Siku ya sita  – 9 Julai, 2022.

Ombi Kuu: Nampigia BABA Magoti.

Neno:  Efeso 3:12-21, Luka 22:40-43.

Ombi la kwanza: Shukrani kwa MUNGU, BABA Yetu;

– Mshukuru sana Mungu kwa Yote aliyokufanyia tangu Januari hadi sasa.

– Mkabidhi Mungu yote yaliyopo mbele yako. (miradi, Kazi, familia n.k.) 

– Mwombe Mungu Kibali kwa majukumu yako.

Ombi la pili: Kuwaombea Wengine

– Mwombe Mungu akupe mzigo moyoni mwako wa kuwaombea wengine (Kol 1:3-5)

– Omba kwa ajili ya kazi ya Mungu ndani na nje ya Tanzania, 

– Kwamba Kanisa lipate watendakazi wenye hofu ya Mungu.

– Kwamba Kanisa likue na kuongezeka kwa maeneo yote. (Kwa idadi, Kiuchumi na Kijiografia)

–  Kwamba Mungu awapake mafuta watumishi wake.

Ombi la Tatu. Ombea Taifa la Tanzania.

– Mwaka wa Serikali 2022-2023 umeanza Julai. Mwombe Mungu atuvushe salama. 

– Mwombe Mungu kuhusu ajira kwa WAHITIMU wote wenye sifa husika.

– Mwombe Mungu kuhusu miradi ya maendeleo inayoendelea ifanikiwe na kukamilika kwa wakati.

Ombi la nne

Ombea Mataifa Mengine.

– Ombea Uchaguzi mkuu Kenya utafanyika August 2022

– Omba Mungu aingilie kati vita vya ndani vilivyopo DRC, Somalia nk

-Omba Mungu aingilie kati vita kati ya URUSI na UKRAINE

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top