SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA. 24 JANUARI 2024 KUOMBEA WATOTO NA VIJANA

KUOMBEA WATOTO NA VIJANA. 

Zaburi 127:3-5, Yoeli 2:28, Hesabu 6:24-26,

1. Ombea watoto wa DPC. Kumb 6:6-7, Kumb 11:18-19, 1 Timothy 5:8, Luka 2:52, Mithali 1:8-9

– Ombea wazazi/walezi wasimame katika nafasi zao katika kuwalea watoto. 

– Ombea shule ambazo watoto wanasoma, Mungu awapiganie na kuwalinda. Zaburi 23

– Ombea walimu na walezi ambao wanakuwa na watoto muda mwingi zaidi.

2. Ombea idara ya watoto kuwahudumia watoto hii katika viwango bora vya juu ili tuwe na kizazi imara yenye viongozi bora katika kipindi kijacho. Mithali 22:6, Kumb 5:29

–  Tuwafundishe watoto wetu maadili mema itakayowafaa katika maisha. Isaiah 54:13, 3 John 1:4

–  Ombea walimu na watendakazi wote wa Sunday school

–  Ombea program za watoto ziweze kuleta badiliko la kweli kwenye maisha yao

3. Omba kwa ajili ya mahitaji ya kimwili na kiroho ya Vijana wetu.

– Ombea Vijana wawe vielelezo katika maisha yao. 1 Timotheo 4:12

– Ombea utumishi kwa vijana, waweze kumtumikia MUNGU. Jeremiah 1:5

– Ombea vijana ambao wako vyuoni Mungu awapiganie, Walioko makazini na Kwenye biashara, Mungu aendelee kuwapiagania na kubariki kazi zao. Kumb 28:1

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top