SIKU YA TANO – SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA

Maombi ya siku 21, Wiki ya kwanza

Siku ya 5, Tarehe 13 January 2023Somo: Kuyaishi Maadili ya Kikristo.

1. Omba makanisa yote yajitahidi kutoa huduma za Kiroho bila kusahau huduma za Kijamii. Mathayo 14:15-21, Wagalatia 6: 9-10

a. Kuhudumia Kanisa kama utakavyojaliwa na Mungu

b. Kuyagusa Maisha ya wahitaji wanaotuzunguka ndani na nje ya kanisa.

2. Omba Hofu ya Mungu ndani ya kila mmoja kuruhusu kazi za Roho Mtakatifu ndani yetu. 1Petro 1;17

a. Matunda ya Roho Mtakatifu. Gal. 5;22-23

b. Maisha yanayompendaza Mungu. Math 5;16

3. Omba tuwe na roho ya kuheshimiana, Kupendana, kuthaminiana, na kuwatii viongozi wetu wa Kiroho , kijamii, Serikali, kisiasa nk. Rumi 13:7-8, 1 Pet 1:22, 1 Pet 4;7-11, Rumi 12:10

4. Omba Umoja wa kweli kuanzia ngazi ya chini hadi juu., 1 Pet 3:8, 

a. Umoja katika kanisa la mahali hadi taifa

b. Umoja katika viongozi wetu wote wa kanisa la mahali hadi Taifa

c. Umoja katika familia zetu. 

      Katika umoja ndipo Mungu anaamuru baraka. Zab 133:1-3

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top