SIKU YA SITA – SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA

Siku 21 za Kufunga na Kuomba: Jumamosi 14th January, 2023.

Ombi Kuu: KUYAISHI MAADILI YA KIKRISTO

1. Omba – Mungu atupe roho ya kukomboa wakati – Waefeso 5: 14-17

– Tukatae kufanya kazi ya Mungu kwa ulegevu na mazoea – bali kwa wakati, haraka na ubora – Yeremia 48:10; Mwanzo 2:15

2. Omba – tuwe waadilifu na waaminifu kwa rasilimali alizotupa Mungu – watu, muda na mali – 1 Wakorintho 4:1-2

– Tukatae roho ya uvivu na uzembe bali tuwe mawakili wema na waaminifu kwa Mungu – Mathayo 25:15-30

3. Omba – Mungu atujaze na kutusaidia kuishi sawasawa na tunda la Roho – Wagalatia 5:22

– Mungu atuongezee imani, atusaidie na kutuvusha salama pindi tunapopita kwenye changamoto za wokovu na utumishi – Luka 17:5

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top