ITAKUWA HERI NA SALAMA KWAKO

ITAKUWA HERI NA SALAMA KWAKO

ISAYA 3:10
Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao

Kama itakuwa heri na salama kwetu, tufanye nini sasa (somo ktk ujumbe wetu)

  • TUMPE MUNGU SHUKRANI

MAOMBOLEZO 3: 22 – 23
22. Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
23. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.

  • Tumshukuru Mungu kwa ajili ya rehema zake zisizokoma kwetu kiasi kwamba hatuangamii
  • Tumshkuru Mungu kwa ajili rehema zake ambazo ni mpya kila siku ili kututunza na kutuokoa  
  • Tumshukuru Mungu kwa ajili ya uaminifu wake kwetu

ZABURI 40: 1-3
1 Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana

  • Tumshukuru Mungu kwa sababu atatutoa katika shimo la uharibu na kutusimamisha mahali salama
  • Tumshukuru Mungu kwa sababu anakwenda kuweka wimbo mpya katika vinywa vyetu (wimbo wa sifa)  

2 TIMOTHEO 4: 16-18
Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. 18 Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.

  • Tumshukuru Mungu kwa sababu anakwenda kusima upande wetu na kututia nguvu
  • Tumshukuru Mungu kwa sababu anakwenda kutuokoa dhidi ya adui  
  • Tumshukuru Mungu kwani atatuongoza ili tufikie ufalme wake
×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top