Siku 21 za Kufunga na Kuomba (13 Januari 2024) HUDUMA ZA KIJAMII NA UINJILISTI

Siku 21 za Kufunga na Kuomba. (13 Januari 2024) Siku ya 6
HUDUMA ZA KIJAMII NA UINJILISTI 

  1. Kila mshirika ajitoe kikamilifu katika kuwahudumia watu wengine. 
    Matendo 6: 1-7, Matendo 9:36 – 42, Wagalatia 6:9-10, Mithali 19:17, Yakobo 2:14-17
    – Mungu akuwezeshe kuwahudumia wahitaji ya watu wanaotuzunguka kwa mfano wazee, wagonjwa, wafungwa, watoto yatima nk. (Injili ya Matendo) 
  2. Ombea miradi ya kuwafikia watu na mahitaji yao hapa DPC na PAG kwa Ujumla. 
    Waefeso 1:17-19, Mithali 29:7, Kumb 15:11

    – Ombea Mradi/Miradi ipate fedha na mahitaji mengine kwa ajili ya kufikia watu wengi zaidi inagusa 
    mahitaji ya watu na jamii kama NCCT n. k
    – Ombea ubunifu, Kanisa liwe na ubunifu katika kuwafikia watu na mahitaji yao. 
  3. Tuombe kwa ajili ya huduma ya Uinjilisti hapa DPC. Mathayo 9:38, Mathayo 28:18-20
    – Tuombe kwa ajili ya watenda kazi shambani mwa Bwana kwa ajili ya kuwafikia watu wengine na injili.
    – Tuombee washirika tuwe na moyo wa kufanya uinjilisti (Mathayo 28:18-20), 
    – Tuombe kwa ajili ya Kila idara ibuni namna ya kufanya uinjilisti ili kuwafikia watu wa rika yao.
    – Kanisa huihubiri injili ya kweli na kwa ufasaha. Waefeso 6:19-20
  4. Tuombe kwa ajili ya huduma ya Uinjilisti PAG Tanzania.
    – Ombea watenda kazi wote kwenye idara hii kuanzia ngazi ya taifa hadi kwenye wilaya
    – Ombea mipango ya uinjilisti mwaka huu ikafanikiwe na ikazae matunda
    – Omba kwa ajili ya mahitaji ya huduma hii ili kufanikisha mipango yao

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top