MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA JUMATANO 6 JULAI 2022

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA: Jumatano 6 Julai, 2022

Ombi Kuu: MAOMBI YA YABESI

“… Lau kwamba ungenibarikia kweli, kweli na kunizidisha hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na ouvu, …”. (1 Mambo ya Nyakati 4: 9-10).

Wilkinson, B. (2000) ameandika: “maombi kama haya hayana msingi wa ubinafisi kama inavyoweza kuonekana, lakini yako kiroho zaidi na kimsingi haya ndio aina ya maombi Baba wa Mbinguni anapenda kusikia”

Tunapoomba maombi ya Yabesi, ni vyema pia kujikumbusha juu ya andiko la – Zaburi 24: 1-2 “Inchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. …”

 Maombi :

1. Kubariki – Kibiblia inamaanisha kuachilia kibali cha kimungu. 

• Ombea baraka za Mungu juu ya maisha yako katika maeneo yote – Torati 28:1-14  

• Omba wema wa Mungu unaoweza kuachiliwa na Yeye pekee uwe juu yetu.

2. Mungu azidishe mipaka yako – furusa nyingi zitokee mbele yako.

• Omba Mungu akuzidishe ili uweze kuleta matokeo chanya na kutimiza malengo yako

  Ombea miujiza ya Mungu juu yako – vitu visivyoweza kutokea katika hali ya kawaida vianze kutokeaa
– Waefeso 3:20-21

3. Mkono wa Mungu uwe pamoja nawe – uweze kuzungukwa na nguvu za Mungu. 

• Omba mkono wa Mungu wenye nguvu ukulinde na kukuongoza – Joshua 4:19-24

• Ombea uwezesho wa Kimungu katika kumtumikia Yeye Mungu – Matendo 11:21

4. Omba Mungu akuepushe na ouvu – Mungu alinde na kuhifadhi maisha yako. 

• Ombea ulinzi wa Mungu dhidi ya nguvu za uovu na uvamizi wa adui – Isaya 54:17

• Omba nguvu na uwezo wa kusimama dhidi ya majaribu ya shetani.  

Ameni.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top